Pwani: Mmoja afariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala na wenzake kuchomwa moto na wasiojulikana

Pwani: Mmoja afariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala na wenzake kuchomwa moto na wasiojulikana

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Mkazi wa Umwerani, Kata ya Kongowe, Kibaha Mkoani Pwani Mrisho Omary amefariki baada ya nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi kuchomwa moto na Watu wasiojulikana akiwa amelala na wenzake ndani.

Watu wengine waliokuwa kwenye nyumba hiyo siku ya tukio May 15,201 ni Mwalimu Ally Shaban na Lusekelo ambapo wote waliwaishwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi na Mrisho akafariki May 17.

RPC Mkoa wa Pwani, Wakyo Nyigesa amesema,

Mwanamke mmoja anaitwa Zuwena alipiga kelele akisema amebakwa na kuibiwa simu na Elfu 30 na Watu hao watatu, Watu hao wakakimbilia kwenye nyumba hiyo ndipo Wananchi wenye hasira kali wakaichoma nyumba moto.

Uchunguzi wa awali unaonesha kulikuwa na ugomvi wa kimapenzi kati ya Zuwena na Watu hao aliowaitishia wizi na upelelezi unaendelea kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo.


Nyigesa.jpg
 
Back
Top Bottom