Mupirocin aka bactroban; sijui jinsia yako wala umri wako na nadhani kama si idea ya mambo ya tiba basi wewe ni mtaalamu wa tiba kwa jinsi ulivyoandika vipimo, diagnosis na dawa ulizotumia. Nitaomba niandike ninayoyajua kuhusu pyelonephritis kwa lugha ya kawaida kwa faida ya wasomaji wote wa jukwaa hili.
Kwa dalili ulizonazo inawezekana kweli ukawa na tatizo hilo la pyelonephritis ambalo ni uambukizo kwenye figo unaosababiswha mara nyingi na uambukizo unaoanzia kwenye njia ya mkojo (UTI) na baadae kupanda juu kwenye figo.
Sehemu kubwa ya uambukizo husababishwa na bacteria hasa aina ya E coli kwa asilimia 75% hivi lakini bacteria wa aina nyingine pia huweza kusababisha pyelonephritis. Lakini zaidi ya maumivu ya tumbo, mtu mwenye tatizo hilo pia atakuwa na homa na maumivu wakati wa kukojoa. Hukueleza kama dalili hizi ulikuwa nazo au la. Saa nyingine hata kutapika.
Zaidi ya pyenonephritis matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha loin pain na homa ni pamoja na mawe kwenye figo (nephrolithiasis), uambukizo kwenye tezi ya kiume (prostatitis), lakini pia uambukizo kwenye kibofu cha mkojo (cystitis - ingawa urinalysis yako ilikuwa normal), kwa wanawake anaweza kuwa na uambukizo kwenye via vya nyonga (PID), saa nyingine hata uambukizo kwenye kidole tumbo (appendicitis).
Ultrasound inaweza kusaidia lakini sidhani kama ultrasound peke yake inaweza ku-diagnose pyelonephritis, ultrasound ingeweza kuonyesha figo zimeongezeka size au kama kuna usaha ungeonekana kama ni majimaji lakini pia kwa ultrasound huwezi kusema kama hayo majimaji ni usaha au majimaji ya aina nyingine kwa kuwa vyote huonekana vyeusi iwe ni maji ya kawaida, usaha, au damu.
Ningekushauri kama unaweza, fanya hata CT scan au MRI hizi zinaweza kuonyesha tatizo vizuri zaidi na ukapata tiba sahihi. Unaweza pia kufanya kipimo cha kuchunguza figo, mirija inayoleta mkojo kwenye kibofu na kibofu yaani KUB (Kidney, ureters and urinary bladder) x-rays ambacho kinaweza kuonyesha mawe kwenye hizi sehemu. Picha kamili ya damu, kama itaonyesha chembe nyeupe zikiwa zimeongezeka inaweza kumaanisha uambukizo mwilini, inaweza kusaidia kidogo.
Dawa ulizotumia ndizo ambazo mara nyingi hutumika kwa ajili ya tatizo la pyelonephritis, lakini kama hukufanya culture na senstitivity ya mkojo au damu, ni vigumu kujua ni wadudu gani wamesababisha huo uambukizo na ni dawa za aina gani zinawatibu. Hivyo unaweza kutumia hizo dawa usipone kwa kuwa wadudu wako resistant kwazo. Hivyo culture ni muhimu.
Ukiwa na mawe tiba yake ni upasuaji. Kama ni uambukizo tiba yake ni antibiotics au na specifically ile itakayoendana na culture na sensitivity results.
Mtafute daktari bingwa wa figo (nephrologist), Muhimbili wapo anaweza kukusaidia zaidi.