Huwa nafurahi nikisikia timu inayochukua ubingwa kila msimu ikitetereka maana hadi mashindano yanakuwa yanaboa, yani hata timu zijipindue vipi ila mwisho wa siku bingwa ni yule yule tu kila msimu hadi mnamchoka akiachia sana ni msimu mmoja au miwili baada ya hapo anaendelea tena, kwa hapa africa ndio huyo al ahly na kwa ulaya tunajua ni real madrid binafsi hizo timu sizipendi na huwa nafurahi sana zikifungwa, msimu huu ikichukua timu nyingine tofauti na al ahly itakuwa vizuri sana na itaamsha matumaini hata kwa timu nyingine, natamani wachukue orlando pirates au hata mamelodi sundowns