Q, Chief: Uwezo wangu kimuziki ni mkubwa sana, Patoranking ameshangaa watanzania kunipotezea

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
1,817
Reaction score
4,061
Msanii wa Bongo fleva wa kitambo Q Chief amedai ana uwezo mkubwa sana kimuziki na hili limethibitishwa alipoomba kolabo na msanii wa Nigeria Patoranking
Anadai alipoomba kolabo na msanii huyo yeye hakutaka fedha aliomba apewe demo na alipopewa demo akapigwa na butwaa juu ya uwezo wa msanii huyo na kushangaa alikuwa wapi kipindi chote hicho
Amesema wasanii wa size yake ambao anatakiwa kukaa nao meza moja ni Patoranking na sio hawa wengine tunaowajua
Ametolea mfano wa mume au mke kuwa na mwenza mzuri ndani na hagundui kuwa ni mzuri bali watu wa nje ndio humuona mzuri
 
Huyu jamaa alikuwa mlevi chakaliiii

Mpaka alikuja kitaa kuweka bond mkufu wake bahati nzr jamaa mmoja hv alikuwa anamkubali sana Q zamani akakubali kumwekea bond,akamsitiri


Q chilla kashajifia mlevi hatari ,maisha yke ya kutanga tanga labda saizi abadilike
 
Ktk wasanii wanaotamani yatokee maajabu ya yeye kurudi,basi ni huyu Q chillah na akipata hiyo bahati, wakina MOND watamtafuta kwa tochi na hawatampata maana anausongo haswa wa kurekebisha makosa yake.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] haavhaaa aiseeee

Hajui km dono ndo anatembelea nyota yake
 
qchillah ,Tid mnyama
wanastahili na sijui kwanini walipotea!!
sikiliza billnass ligi ndogo ,chorus [emoji119][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
mdogo mdogo ya qchillah[emoji91][emoji91]
mkungu wa ndizi[emoji91][emoji91][emoji91]

sauti zao dhahabu sana!! acha wajivunie
 
Kimuziki yupo fresh ila wabongo sio mara zote huwapa watu nafasi ya pili.

Ushapewa chance ukizingua ndio imetoka.Aendelee Kukaza pengine atapata nafasi ya pili ila aache unga kikweli kweli sio kujidanganya mwenyewe.

yote kwa yote ngoma yake kali sio utani.
 
Q-Chief ulikuwa Vizuri Sana ila Ngada ndio iliyokumaliza,Piga kazi utatusua tu maana wewe ni msanii,Nikikumbuka mipini uliyopiga chorus enzi hizo MPIGA DEBE,KAMA UNATAKA DEMU.Ukija kwenye Pini la I'm a Dreamer ni soo.
 
Yeye na Tid wanajua saaana kinamuangusha pombe na unga!!
 
Q Chief ni moja ya wanamuziki ambao niko tayari kununua kazi yake kwa vyovyote.Anakipaji kikubwa mno na nyimbo zake huwa hazinchoshi
 
Nimeukumbuka huu mstari wa Nay wa Mitego katika mziki gani;
"Muziki wenu ushirikina ndio umetawala, q chilla analalama anasema umemroga
Mganga wako aliekutoa umemkimbia hujamlipa, bila skendo za magazeti basi huskiki"
 
Q-Chief ulikuwa Vizuri Sana ila Ngada ndio iliyokumaliza,Piga kazi utatusua tu maana wewe ni msanii,Nikikumbuka mipini uliyopiga chorus enzi hizo MPIGA DEBE,KAMA UNATAKA DEMU.Ukija kwenye Pini la I'm a Dreamer ni soo.
Ongeza yupo na jaydee sitaki kumbuka zamani(sitaki ota) hapo ilikuwa khatari sana mpiga debe akiwa na mzimuni family wacha kabisa ndugu umenikumbusha kitambo kidogo hiyo.
 
Ongeza yupo na jaydee sitaki kumbuka zamani(sitaki ota) hapo ilikuwa khatari sana mpiga debe akiwa na mzimuni family wacha kabisa ndugu umenikumbusha kitambo kidogo hiyo.
Aisee hiyo Pini Q-Chief aliua mbaya,Walaaniwe wazungu wa Unga,[HASHTAG]#Amani[/HASHTAG] kwa kaka voda milionea waambie wadogo zako waache poda wale mmea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…