Qatar kombe la dunia 2022

Joined
Sep 8, 2022
Posts
2
Reaction score
16
DEJAN STANKOVIC NA HISTORIA YA PEKEE YAKE WORLD CUP..

Mchezo wa soka ndiyo mchezo mahususi na unaopendwa zaidi miongoni mwa michezo yote ya kiushindani Ulimwenguni . Kila baada ya miaka minne hufanyika michuano ya kombe la dunia , kwa upande wa wanaume ndiyo huvutia sana mashabiki .

Zikiwa zimesalia siku 66 kuelekea fainali za kombe za kombe la dunia "FIFA World Cup" hebu tuwekane sawa kwa hili la huyu mwamba .

Michuano ya kwanza ilifanyika mwaka 1930 huko nchini Uruguay , mwaka huu fainali za kombe la dunia zitafanyika nchini Qatar itakuwa ndiyo ya kwanza kufanyika Uarabuni .

Idadi ya timu zitakazo shiriki ni 32 , timu 5 kutoka Afrika , 5 kutoka Asia , 1 kutoka Oceania , 5 America kusini , 3 kutoka America kaskazini na 13 kutoka Ulaya .

Kwa mujibu wa sheria zilizopo mchezaji hapaswi kuwakilisha taifa zaidi ya moja , hata ikiwa amebadilisha uraia wa taifa moja na kupewa lingine hatokuwa na kibali cha kuchezea taifaalilopewa uraia .

Sheria iliyopo ni endapo Jacinta ukawa umezaliwa England lakini una asili ya Jamaica utaweza kuchagua kuchezea moja kati ya mataifa hayo mawili , kigezo cha timu uliyoichezea nacho huangaliwa kwa mfano ufuatao ; Jacinta upo na uraia wa England na ukachezea timu yao ya taifa kwa ngazi ya Under 16 , Under 17 , Under 18 mpaka Under 23 bila ya kuchezea Senior team utaweza kuswitch kutoka England na kuichezea Jamaica .

Kama umeshaichezea senior team ya England mechi zaidi ya 3 lakini ni za kirafiki bado utaweza kuichezea Jamaica lakini kama umeichezea England kwenye mechi zaidi ya 3 za kiushindani basi hautoweza kuitumikia Jamaica milango itakuwa imefungwa mazima na siyo kwenye world cup bali kwenye michuano yryote ile .
NB. Mfano huo ni kwa mataifa yanayoruhusu uraia wa nchi mbili kwa Tanzania yetu haiwezekani kuwa Mtanzania halafu pia ni Mnigeria .

Lakini sasa kuna huyu Anko anaitwa Dejan Stankovic yeye alichezea timu tatu tofauti kwenye World Cup tofauti na hakuzuiwa kivyovyote vile .

Mwaka 1998 wakati World Cup ikifanyika nchini Ufaransa , Dejan alikuwa akikitumikia kikosi cha timu ya taifa ya Yugoslavia alikiwa kikosini kabisa na michuano alishiriki , ilipotimu mwaka 2003 serikali ya shirikisho ya Yugoslavia ilisambaratika na mataifa kujipatia uhuru .

Miongoni mwa mataifa yaliyojiengua kunako taifa la Yugoslavia lilikuwepo Serbia & Montenegro , Bibi wee! Ile kufika mwaka 2005 taifa la Serbia & Montenegro likafuzu kushiriki fainali za mwaka 2006 zilizofanyika nchini Ujerumani na Dejan alikuwa tayari ni raia wa Serbia & Montenegro hivyo akaitwa kikosini na akashiriki michuano hiyo akiwa mchezaji wa Serbia & Montenegro tena Captain wao .

Baada ya mivurugano ya kisiasa hatimaye Serbia & Montenegro zikajitenga na kuwa mataifa yanayojitegemea Serbia kivyake na Montenegro kivyao .

Guess what! Kwenye michuano ya mwaka 2010 iloyofanyika nchini Afrika Kusini jamaa Dejan Stankovic aliitwa na kuitumikia timu ya taifa ya Serbia kama taifa lake na hatimaye kuweka rekodi yake ya kipekee ya mchezaji mmoja mmoja kutumikia mataifa matatu kwenye michuano mitatu tofauti .

Kuna legend wengi walifanya makubwa sana lakini huyu Dejan ameacha historia ambayo ni ngumu sana kwa leo hii kufikiwa sembuse kuvunjwa . Ahsante Sana!
 
R. I. P Yugoslavia. Marekani murdered you.

Anataka tena kuiua Serbia ili izaliwe Kosovo dadeq dejan angendelea kuwepo kweny soka mbona angecheza mataifa hata matano tofauti.

Lkn Russia 🇷🇺 yupo macho anatizama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…