Uchaguzi 2020 Queen Sendiga (ADC): Mgombea atakayeshinda Urais asiwasahau wenzake

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ADC, Queen Sendiga amemshauri mgombea atakayeshinda kutowaweka kando wagombea wenzake walioshiriki kinyang’anyiro hicho.

Mgombea huyo amesema Serikali shirikishi ndiyo chanzo cha maendeleo, hivyo ni vema Rais atakayeshinda akawaweka karibu washindani wake, ili kupata mawazo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2020 amesema licha ya kuwa dhamira ya ADC ni kuchukua dola, anatambua mgombea atakayeshinda ni mmoja hivyo anaweza kuwa yeye au wa kutoka chama kingine.

Sendiga ameeleza kuwa endapo atashinda yeye, atazitumia ilani za vyama vyote hata kwa kuchukua mambo machache.

“Mgombea atakayefanikiwa kuchukua kiti cha Urais, washauri wake wa kwanza wawe watu ambao ameshindana nao, kwani Serikali shirikishi mara nyingi huleta matokeo mazuri na ya haraka katika jamii,” amesema.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] amefanya vema kutoa angalizo
 
Lissu hafai hata kwa bure, aende zake Ubelgiji kwa beberu wake hiyo 18/12.
 
Mawazo/Ushauri mzuri, ila Rais mtarajiwa hufuata ushauri mwema achana na huyu asiyeshaulika. Kura kwa Mh: Tundu Lissu.
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ADC, Queen Sendiga amemshauri mgombea atakayeshinda kutowaweka kando wagombea wenzake walioshiriki kinyang’anyiro hicho.

Mgombea huyo amesema Serikali shirikishi ndiyo chanzo cha maendeleo, hivyo ni vema Rais atakayeshinda akawaweka karibu washindani wake, ili kupata mawazo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27,2020 amesema licha ya kuwa dhamira ya ADC ni kuchukua dola, anatambua mgombea atakayeshinda ni mmoja hivyo anaweza kuwa yeye au wa kutoka chama kingine.

Sendiga ameeleza kuwa endapo atashinda yeye, atazitumia ilani za vyama vyote hata kwa kuchukua mambo machache.

“Mgombea atakayefanikiwa kuchukua kiti cha Urais, washauri wake wa kwanza wawe watu ambao ameshindana nao, kwani Serikali shirikishi mara nyingi huleta matokeo mazuri na ya haraka katika jamii,” amesema.
Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.
Pasco
 
Back
Top Bottom