Uchaguzi 2020 Queen Sendiga aendelea leo na Kampeni za Urais jijini Dar esSalaam kwa kumuenzi Baba wa Taifa

Uchaguzi 2020 Queen Sendiga aendelea leo na Kampeni za Urais jijini Dar esSalaam kwa kumuenzi Baba wa Taifa

ADC Party

Member
Joined
Sep 14, 2020
Posts
28
Reaction score
29
Leo mgombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kupitia chama cha ADC ameendelea na kampeni zake katika Viwanja vya Bakhresa Manzese ,Jimbo la ubungo.

Leo ni siku ya furaha na masikitiko pia kwa taifa zima,watanzania wote kukumbuka siku ambayo Baba yetu wa Taifa Julius Kambarage Nyerere alitutoka , katika kipindi hiki tunachoenda kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo kwa nchi yetu kwa miaka 5 ijayo tunakumbuka vipi na kutekeleza yale aliyokua akiyapigia kelele kila siku.

"Nakumbuka Baba wa Taifa wakati tu tumepata uhuru wetu kutoka kwa wakoloni alisema sasa tunaenda kupigana vita nyingine na maadui 3 katika taifa letu.

"Ujinga, maradhi na Umaskini, Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, kama na aliongeza pia kama baadae Tanzania itafanikiwa kuyamaliza basi itakua miongoni mwa nchi itakayoendela zaidi duniani."

Ni mbaya zaidi mpaka sasa bado tunapigana na maadui hawa watatu na hali inazidi kutokua nzuri kwenye maeneo mengi na kuonekana njema kwa maeneo machache hasa ya mijini , ndio kwa sababu chama cha ADC na mimi leo niliyesimama mbele yenu nimewaletea vipaumbele vikubwa 3 ambavyo bado vinamashimo makubwa ya utekelezaji tokea baba wa taifa alivyopiga kelele mpka leo ambavyo ni Elimu, Afya na Kilimo.

Kwa kuweka mifumo bora ya utekelezaji kwa yote niliyowaelezea nawaomba tarehe 28 mkanipe kura za ndio ili mimi na nyinyi tukaingie kwenye vita ya kupigana na hawa maadui 3 ili alipolala Baba yetu wa Taifa aweze kufurahi na kuona sasa watanzania neema imewafikia.

Pia mgombea akasisitizia suala la miundo mbinu kua mibovu kwa kutolea mfano mvua zilizoikumba dar es salaam siku jana na kusababisha maafa makubwa , chagueni viongozi ambao wataenda kuhakikisha kazi hasa za lazima zinafanyika na sio mihemko na kujikuta kila mwaka tupo kwenye tatizo lile lile " aliyasema haya leo mapema katika viwanja vya bakhresa manzese katika kampeni zake.

Lakini pia aliweza kupata muda kumnadi mbunge wa jimbo la Ubungo ,Bi Zuwena Mohammed Abdallah na mgombea huyo akapata machache ya kusema.

" nitahakikisha machinjio ya masoko kwenye Jimbo lake yanakuwa ya kisasa ili kuongeza ufanisi. Na pia atashughulikia miundo mbinu Jimbo la Ubungo eneo kubwa halifikiki hasa katika msimu wa mvua" Alisema Bi Zuwena.

Mgombea Urais ataendelea na Kampeni zake keshokutwa Mkoani Iringa.

Imetolewa na
Devilsi Method
Kampeni Manager

1626269673.jpg
267898774.jpg
1131641586.jpg
1496021915.jpg
1738112390.jpg
 
Back
Top Bottom