ADC Party
Member
- Sep 14, 2020
- 28
- 29
Moja ya mikoa iliyobarikiwa ardhi yenye rutuba na Hali ya hewa ya kurutubisha mazao ya biashara kama nyanya,vitungui,mahindi na mbogamboga ni Iringa, lakini mazao haya yanaonekana maeneo mengi ya mashambani na sokoni yakioza kwa kukosa soko la kutosha na hii inazidisha Hali ya umaskini kwa mkulima wa iringa. Mh Queen amesema endapo.
Watanzania wakitupatia ridhaa ya kuongoza nchi hii ifikapo 28/10/2020 tunakwenda kujenga viwanda vya kutosha kulingana na uzalishaji uliopo mkoani hapa ili kuongeza tija kwa wakulima na ajira wa Wana Iringa.
Mh Queen pia ameomba wananchi wa Jimbo la Iringa mjini kumchagua mgombea Ubunge wa ADC Mh Daudi Issa Masasi ili aweze kutekeleza Ilani ya chama cha ADC.
Pia amewakumbusha watanzania kutumia Hali yao ya kikatiba kuchagua viongozi hivyo wajitokeze kwa wingi kupiga Kura ifikapo tarehe 28/10.
Mh Queen anaendelea na ziara zake za lala salama katika mkoa wa Singida, aliporudi kukamilisha ratiba kutokea na kushindwa kuzifanya week iliyopita kutokea vurugu zilizotokea. Ameongea haya akiwa Stand ya zamani , Iringa Mjini.