ADC Party
Member
- Sep 14, 2020
- 28
- 29
Mkoa wa Tanga ni moja ya miji mikongwe na yenye kila aina ya rasilimali.
Ukiacha ardhi Bora,madini, bahari misitu ya asili mkoa wa Tanga ni maarufu kwa zao la mkonge,licha ya umaarufu wa zao Hilo na faida zake kwa wakulima na Taifa bado wananchi wa mkoa wa Tanga hawana faida na mkonge kwa miaka mingi sasa
Endapo ADC itapata ridhaa ya kuongoza nchi hii kupitia sera yake ya maboresho ya kilimo kww mtanzania itaenda kurudisha hadhi ya zao la mkonge,kwanza itarejesha mashamba kwa wananchi ambayo kwa sasa yako kwa watu binafsi waliokodishwa na mamlaka za mkonge,hii itasaidia kumfanya mkulima apate uhakika wa kipato baada ya kuvuna,ajira zitaongezeka na pato la mkulima,mkoa na nchi litaongezeka.
Lengo ni kuboresha maisha ya watanzania katika kila sekta
Queen Sendiga mgombea urais kupitia chama cha ADC ameyasema hayo akifunga kampeni zake mkoa wa Tanga wilaya ya handeni kunadi Ilani ,Sera za ADC na kuomba watanzania wamchague ili apate nafasi ya kuwatumikia,Queen ameongea na wananchi wa Michungwani, Kabuku,Komkonga ,Mkata na Manga
Pia amesisitiza vipaumbele vya ADC Elimu,Afya na Kilimo kwamba ndio dira ya kumfikisha mtanzania katika mabadiliko ya kimaendeleo na kiuchumi
Pia amemnadi mgombea Ubunge Jimbo la handeni vijijini Mh Doyo Hassan Doyo na kuwaasa wananchi wa Handeni kuacha kuchagua vyama kwa mazoea.
Queen anaendelea na kampeni zake mkoa wa Dar es Salaam na kesho atakua wilaya ya Ilala.