Uchaguzi 2020 Queen Sendiga: Nikichaguliwa kuwa Rais, nitamaliza kero za wakulima wa Korosho

Uchaguzi 2020 Queen Sendiga: Nikichaguliwa kuwa Rais, nitamaliza kero za wakulima wa Korosho

ADC Party

Member
Joined
Sep 14, 2020
Posts
28
Reaction score
29
7E041F0D-70B9-4C75-803D-9A80AF9389BB.jpeg

D15346A7-6123-488E-BEEF-7D92D6C7B5B6.jpeg

4E2A96CB-1D25-47A0-A72E-7332684EDD4C.jpeg


"Nikipata nafasi ya kuwa Rais, suala la changamoto kwa wakulima wa korosho kwa muda mrefu litaisha. Nitahakikisha pembejeo bora zinapatikana kwa wakati.

Kupatikana kwa masoko yasioingiliwa na Utawala:

Kupitia ILANI yetu juu ya kuendesha Uchumi wa Kijiditali; manunuzi yatakua ya kidigitali ambapo kutakuwa na ushindani wa wazi - upatikanani wa Pembejeo kwa wakati na bei muafaka itawezekana ni uboreshaji wa mfumo tu.

Bei ya korosho itakuwa wazi hivyo wakulima watapatiwa fursa ya kuuza korosho yao ama kuitia Ushirika au kwa wanunuzi moja kwa moja ili mradi wameshindwa Zabuni ya wazi na wakulima kupitia vyama vyao wameridhika;

ADC itatathmini upya makato na kodi gandamizi wanayokatwa wakulima ili kuona kama inatija au laa.

Wauza bidhaa nyingine hawaingiliwi kati kwanini wakulima na mazao yao waingiliwe na kupangiwa bei? " - Mgombea Urais Bi Queen Cuthbert Sendiga akiongea na wananchi wa wilaya ya Lindi, kijiji cha Mtama.
 
Back
Top Bottom