Uwazi ktk ndoa ni muhimu, kama mchangiaji mmoja aliposema uwe na mwenza wako, then anapigiwa simu, anainuka na kwenda kuisikilizia mbali nawe, hapo utawaza vibaya tu?. Na mara nyingi hii huwa mifumo dume, mfano utakuta mtu hataki kabisa mke wake ajue kipato chake halisi, lakini kipato cha mke lazima kijulikane.
Tukija kwa suala la barua, hii inatakiwa kuwa wazi. Wote muwe na tabia baada ya kufungua barua yako kumshirikisha mwenza wako baada ya kuisoma. Lakini hata kama mnashirikishana kwa barua, haitakiwi mmoja kufungua barua ya mwenzake, bali inatakiwa kusubiri mpaka mwenye (mme ama mke) barua aifungue na kuisoma ndio mshirikishane. Kwa nini nasema hili, kuna barua inabidi mmoja akishafungua asimpe mwenza wake bali amueleze contents tu kwa kifupi, mfano "Mama anatatizo la afya, anahitaji fedha kiasi kadhaa...", si vizuri mme kujua ugonjwa wa ndani wa Mama (mkwe wake), hasa magonjwa ya siri ya kijinsia na hivyo hivyo mme akisoma baadhi ya barua atamwambia mke wake "Baba amepatwa na maradhi ya kijinsia, hivyo anahitaji msaada". Sio lazima uutaje huo ugonjwa kwa mke.
Pia kabla ya Ndoa ni vizuri kuwekana wazi, kila mtu aseme anafikiria nini kupata toka kwa mwenzake, ili tangu mwanzo muwekane sawa, kuwa hili linawezekana, lile haliwezekani. Ama hapa tutafanya hivi, kusubiri kuja kuyaongelea masula fulani fulani baada ya ndoa huwza kuleta tafsiri ya kuchokana. Kuna watu wako ndani ya ndoa ndio unaanza ugomvi kuwa wapate watoto wangapi, mume anataka 6, mke anataka 2. Hivyo bora kuwekana sawa mapema kwa yale mtakayokumbuka kabla ya ndoa.