QUOTABLE QUOTES OF MWL JK NYERERE by Christopher Liundi

Moony

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2011
Posts
1,599
Reaction score
436
Quotable Quotes of Mwl. JK Nyerere : Collected from speeches and writings. Publisher ni mkuki na nyota.

Kitabu hiki ni kizuri sana ambacho kinafaa kisomwe na kila mtanzania ambaye hakujaliwa kusoma vitabu vya Mwalimu.

Ni mkusanyiko wa mawazo na misemo kutoka katika hotuba za mwalimu wakati wa uhai wake.

Swali langu ni hili:

Je Mwalimu na familia yake wamenufaika vipi kutokana na kuchapishwa kitabu hiki?
Je mawazo ya Baba wa Taifa, hotuba, vitabu,namajarida hayana Intellectual Property rights?

Siku hizi kuna watu wanajitafutia umaarufu na utajiri kupitia jina la Mwalimu Nyerere.

Je MH. Makongoro hili swala unalisemea nini? Mama Maria na familia yote ya Mwalimu munafaidika vipi kutokana:

Uwanja wa ndege wa kimataifa, Chuo cha Kivukoni n.k

Mwalimu Nyerere ni jina takatifu, si la kutumiwa ovyo ovyo tu nanyi watoto mmekaa kimya na mafisadi yanatajirikia kwenu.
Sijui kama Mh Liundi alipata ruksa kutoka wapi wa kuchapisha mawazo ya Baba wa Taifa halafu pesa anaweka mfukoni.

Naomba kujua kama familia, mwalimu Nyerere Foundation na Tanzania kwa ujumla kama wamepata share yoyote.

Naomba kufahamishwa na ikibidi TAMKO rasmi litolewe ili tujue kama hili jina tukufu linaweza kutumika hovyo hovyo kutengeneza pesa.

Naomba KUWAKILISHA:disapointed:
 
Tatizo sijui kama huwa wanaingia JF ....wao ndio wenye majibu ingawa Mwalimu angekuwa hai leo wala asingejali hiyo Copyright kwakuwa kwake ilikuwa Taifa kwanza..
 
Dondosha hayo ma qoutes jamvini, mfano

IMF international ministry of finance
 
Hili Jina Tanganyika nimetafuta sijui limetokea wapi.
 
Ni kweli hapa kwetu Bongo copy right haina maana yoyote. Hata ikiwepo usimamizi ni kikwazo sana. Ni ngumu maana sheria nyingi hazifuztwi.
 
"dhambi ya ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya mtu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…