TANZIA R.I.P Mwalusako

TANZIA R.I.P Mwalusako

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
2,949
Reaction score
1,940
Habari zilizotufikia muda huu mchezaji wa zamani wa team za Taifa, Pan Africa, Yanga, Lawrence Mwalusako amefariki alfajiri hii katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili

====

Alikuwa beki shupavu amezichezea timu kadhaa nchini ikiwemo Waziri Mkuu ya Dodoma, Pan African na Yanga

Mwaka 1986 kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kucheza soka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikinolewa na Joel Bendela

Alisataafu kucheza soka ya ushindani mwaka 1991 akiwa na klabu ya Pan African alisifika kutokana na aina ya uchezaji wake, wa kumudu kucheza vyema nafasi zote za ulinzi

Mwalusako baada ya kustaafu kucheza soka ya ushindani amejihusisha na uongozi katika klabu kongwe nchini ya Yanga akiwa kama Katibu mkuu wakati wa Mwenyekiti Imani Madega na mara ya pili akikaimu nafasi hiyo mwaka 2012 baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Celestine Mwesigwa kusimamishwa

Nyota huyu baada ya kuachana na kazi za uongozi katika klabu ya Yanga hivi sasa alijikita katika shughuli za kutoa ushauri wa masoko ‘Marketing Consultation’ akifanya shughuli hizo hapa jijini, lakini kwa sababu mchezo wa soka uko kwenye damu yake bado anatoa msaada wa ushauri katika klabu yake ya zamani ya Yanga iliyo na maskani yake makuu mtaa wa Jangwani na Twiga
 
... lile dude baada ya kutupumzisha kwa muda limeibuka tena? Au ndio kipindi cha pili kimeanza.
 
Pole nyingi sana kwa Watani zangu wakubwa Yanga SC na kwa Familia ya Marehemu, ila isije ikawa Klabu imemtanguliza ili tu wachukue ASFC!
 
Habari zilizotufikia muda huu mchezaji wa zamani wa team za Taifa, Pan Africa, Yanga, Lawrence Mwalusako amefariki alfajiri hii katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili

====

Alikuwa beki shupavu amezichezea timu kadhaa nchini ikiwemo Waziri Mkuu ya Dodoma, Pan African na Yanga

Mwaka 1986 kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kucheza soka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikinolewa na Joel Bendela

Alisataafu kucheza soka ya ushindani mwaka 1991 akiwa na klabu ya Pan African alisifika kutokana na aina ya uchezaji wake, wa kumudu kucheza vyema nafasi zote za ulinzi

Mwalusako baada ya kustaafu kucheza soka ya ushindani amejihusisha na uongozi katika klabu kongwe nchini ya Yanga akiwa kama Katibu mkuu wakati wa Mwenyekiti Imani Madega na mara ya pili akikaimu nafasi hiyo mwaka 2012 baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Celestine Mwesigwa kusimamishwa

Nyota huyu baada ya kuachana na kazi za uongozi katika klabu ya Yanga hivi sasa alijikita katika shughuli za kutoa ushauri wa masoko ‘Marketing Consultation’ akifanya shughuli hizo hapa jijini, lakini kwa sababu mchezo wa soka uko kwenye damu yake bado anatoa msaada wa ushauri katika klabu yake ya zamani ya Yanga iliyo na maskani yake makuu mtaa wa Jangwani na Twiga
Yaani mkuu mtu ameshafariki bado wewe unaandika "....bado anatoa msaada wa ushauri katika klabu yake ya zamani ya Yanga..."?
 
Acha hizo...ndiyo nyie mnaosemwa mnasambaza uongo...huyu comrade Alikuwa na matatizo muda mrefu...Tena nimedokezwa Alikuwa amefanyiwa operesheni
Hakukua na sababu ya kueleza alikua anafanya nini kwa sasa.
Watu wanalazimika kujua ni nini kimekatisha uhai wake.

Yanga mnakwama wapi?
 
Back
Top Bottom