Radi yaua wanawake watatu

Radi yaua wanawake watatu

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mmoja alikumbwa na mauti wakati akikinga maji ya mvua nje ya nyumba yake wakati wawili walikuwa wakitoka shambani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alisema tukio la kwanza lilitokea jana saa 12 asubuhi katika Kijiji cha Kisaki kituoni wilayani Morogoro, ambapo mwanamke mmoja mkulima, Maua Kibamba (22), alifariki dunia wakati akikinga maji ya mvua.

Maua alipigwa radi na kuungua upande wa kushoto wa mwili wake na kufa papo hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, tukio lingine lilitokea juzi saa 2 usiku katika Kijiji cha Dunduma, Kata ya Sungaji Tarafa ya Turiani wilayani Mvomero, ambapo wanawake wawili walikufa kwa kupigwa radi wakitokea shambani.

Mutafungwa alieleza kuwa wanawake hao waliungua maeneo mbalimbali kabla ya kufariki.

Mutafungwa aliwataja wanawake hao ni Dativa Nyego(60), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kichangani na Shukuru Samnyau (28), mkazi wa Kijiji cha Dunduma.

Alisema miili yao imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu zaidi za mazishi.

Alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kujiepusha na athari za mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ikiwamo kuepuka kukaa chini ya miti mikubwa na maeneo ya wazi ili kupunguza madhara ya radi.

Wakati huo huo Polisi wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kukamata pikipiki tatu zilizodaiwa zilikuwa zikitumiwa na watuhumiwa katika shughuli za utapeli.

Mutafungwa alisema watu hao walikuwa wakifanya utapeli katika maeneo ya vijiji vya Rudewa na Msowero wilayani Kilosa na walibainika baada ya upelelezi uliofanywa na jeshi hilo.

Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakiwatapeli wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani, kwa kuwauzia nafaka hewa ambazo ni mchele, mahindi na maharage kwa kuwahadaa kwamba ni mali ya wizi ambazo zinauzwa kwa bei nafuu.

Alisema watu hao walikamatwa katika misako mbalimbali iliyoendeshwa Novemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Waliokamatwa ni Selemani Fadhili (52), Omary Mohamed (30), Limamu Jackson (28), Mussa Manguture (33), Mfaume Omary(33), Hamadi Kassim (20) na Said Shabani (38) wote wakazi wa Rudewa. Wengine ni Christopher Sprian (25), Shauri Mohamed (42), Abdallah Bakari (45) na Abdallah Mussa (24), wakazi wa Kijiji cha Msowero.
 
Pole yao..,

Tujiwekeze kwenye Technologia ya kufua umeme wa radi.. Utumike kama ilivyo kwa solar
 
Ina Lila wa ina Lila wa ina Lila wachina ila raijun
 
Back
Top Bottom