Radio Clouds na Anguko la Elimu na maanadili nchini

Radio Clouds na Anguko la Elimu na maanadili nchini

Eastern Arc

Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
6
Reaction score
1

Nakumbuka mwaka jana yalipotangazwa matokeo ya Form 4 kuna kijana mmoja aliyefanya mtihani huo ikaonekana badala ya kujibu maswali yeye alijikita zaidi kwenye kuandika mistari (tungo za bongo flava). Hii kitu ilivuma sana na ilikuwa mshangao mkuu kwa Taifa hili changa.

La ajabu na kusikitisha sana, hii Radio ya mtaani, CLOUDS FM, hapa namaanisha akina Hando na mdada wake, wakamwalika kijana huyo na kuanza kumhoji katika mtindo wa kumuunga mkono. Waling'ang'ania sana kuwa ati umefika wakati kwa nchi na wazazi kwa ujumla kuangalia vipaji vya watoto na si kulazimisha vitu ambavyo watoto hawaviwezi,,,kufanya mtihani wa FM4! Walienda mbali zaidi kwa kushauri kuwa iwepo njia ya kutambua vipaji vya watu kama cha huyo kijana ambavyo vinastahili kuendelezwa bila kujali kama amefika form four au la. Watu kadhaa, maskini, waliingia mkenge nakuanza kumuunga mkono huyo kijana wa kitendo chake cha kuandika mistari! Sasa, mimi nadhani;

1. Kwa wakati huu wa science na technologia kuchambua na kujadili vitu kama hivyo ilikuwa ni sawa na kuwasha moto kwa vijana wengine waliokuwa wanasikiliza. Haishangazi kabisa kuona, mwaka huu badala ya mtu mmoja, vijana wengi waliofanya mtihani wamejiingiza katika matendo ya kuandika mstari. Kuna taarifa kuwa baadhi ya vijana walikuwa na akilisana na kama wangejikita kwneye mtihani sawa sawa wangeweza faulu. CLOUDS FMhaiwezi kukwepa lawana zote kwa hili.

2. Sijajua na wengi hawajui, kiwango cha shule walizonazo hao watangazaji. Labda inaweza kuwa ndiyo sababu ya kutoa habari ambazo mara nyingi sana zinakuwa sizo (wrong information) ambazo zinachangia sana kuwafanya vijana wa kibongo waendelee kuwa mbumbumbu kila kuchao. Kwa hili nawakumbuka watangazaji wa siku za nyuma wa kipindi cha PB (majina nimesahau) kwa jinsi walikuwa na makini sana.

3. Ifikie wakati hizi Radio stations zijitathimini zenyewe. Kwa mfano, wengi tunatambua kuwa Radio kama Clouds FM ni ya kufurahisha (entertainment) na sikuhabarisha. Hii inatokana na historia yake. Hatujawahi sikia kama kuna mtu ndani ya hiyo Radio mwenye taaluma ya habari katika kiwango hata cha chini cha Diploma. Tumeshudia mara kadhaa kuanzia enzi za akina Marehemu Amina Chifupa ambapo alikuwa anaweza akaanzisha topic ambayo siyo kabisa (off point) na watu kadhaa wakachangia na kupotelea humo. Na hii inajirudia mara nyingi sana siku hizi hasa asubuhi wakati PJ anasoma magazeti kwa umakini lakini Hando anaingilia kati na kuanza kuvuruga kabisa mwelekeo wa habari husika kwa kutoa mawazo (comments) yaliyo nje (off point) kabisa. Hapa sijamwongelea yule dada/mama wa Usiku kuanzia saa nne jinsi anavyoongea kama kwamba anayesikiliza na boyfriend wake! Hii kitu inachangia sana kushusha elimu yaWatanzania, hasa form 4 na form 6 ambao hawasomi vitabu bali kusikiliza radiona music. Mambo ya habari wawaachie TBC, ITV, Star-TV, Daily News, Guardian nawenzao ambao wamewekeza vilivyo huko.

4. Mwisho na muhimu sana, owners wa Radio kama hizi lazima warudi na kusimamiakwenye malengo yao ya awali walipoanzisha hizo radios. Kama waliamua kutoajiriwasomi waliobobea kwenye habari na lengo ni kuwapata wasikiliza wa namna hiyohiyo, wabakie hivyo hivyo. Hii issue ya kupotosha habari ni sawa kabisa kabisana mgomo wa waalimu au uhaba wa vifaa vya kufundishia ambao unaepeleka elimukushuka nchini.

 
Back
Top Bottom