Hii Radio huwa natafakari imeanzishwa kukashifu dini zingine au lengo lake hasa ni nini??
Leo Asubuhi nimesikia wakizungumzia mchakato wa katiba mpya. Jambo ambalo wamelipa kipaumbele katika mazungumzo yao ni kuhusu maoni ya waislamu kutoa maoni yao kwa kuomba mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC jambo ambalo mimi binafsi sikuwa na tatizo na hilo, ila mashaka yangu ni pale walipoingiza masula ya kuwa wakristo wao hawakupeleka maoni bali walienda kupinga mahakama ya kadhi na kujiunga na Islamic country. Pia wakadai kuna chuo kimoja ambacho ni cha wakiristo wamefanya kikao na wasomi wa kikristo kujiandaa kwenda kupinga kuhusu mahakama ya kadhi na n.k!! Swali langu kwao wao kama wao lengo lao ni wakristo kuwazuia maoni yao kwa mantiki kwamba tume imeundwa kwa ajili ya kupokea na kukubali. Mimi nawaomba wajipange, wahamasishe waislamu kuchangia katika kujenga mashule, miradi na kushirikiana na dini zote ili kuleta umoja. Mfano ukienda leo St Augustino mpaka kuna msikiti pale, ukienda kule Bukoba asilimia 80% ya hospitali ni za makanisa na wanatibiwa watz wote ukienda pale huulizwi we dini hapana, serikali imesecond watumishi wa kila aina lakini wao leo pale Morogoro kwenye chuo wameweka masharti magumu mno kiasi kwamba Mkristo atashindwa kujiunga pale au kufundisha na ndio maana chuo kinalegalega lakini wakifanya chuo kiwe imara wapunguze masharti lakini zile nyadhifa za juu ziwe kwa wasomi waislamu.
Tutafakari sisi sote ni Watz, suala la udini halitatufikisha popote. Hivi leo hii mkuu wa NECTA akiwa muuislamu wewe kama muislamu utaifaidika nini kwenye maisha yako ya kila siku, hata akiwa mkiristo wewe kama mkiristo utafaidika na nini, mfano mkapa alikuwa rais je wakiristo wa kawaida tumefaidika nini, ametujengea nyumba la hasha.
Tutafakari.