Radio Maria Tanzania tengenezeni vitega uchumi

mchecheto

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2014
Posts
1,532
Reaction score
1,462
Habarini wanajukwaa?
kwa wale wakatoliki hii itatugusa zaidi.

Ni ukweli usiopingika kwamba hii radio station inayoitwa Radio Maria inafanya kazi kubwa kuinjilisha kwa njia mbali mbali kama mafundisho ya imani,nyimbo nzuri za dini,tafakari ya biblia nk.
Kituo hiki kinaendeshwa na michango ya waumini.

Kero yangu:
Hiki kituo kila saa ni matangazo ya kuomba michango ya kukiendesha .Hakuna mpango wa kutengeneza michango ya kukiendeleza na sidhani kama ipo.

Maswali yangu?
1.Kwanini hii radio station isirndeshwe kibiashara kama zilivyo nyingine ili kuniendesha bila kutegemea michango?

2.Kwanini wasifikirie kujenga vitega uchumi ili kukidhi garama za yendeshaji badala ya kutegemea 50 za waumini?

3.Mbona wasiige mfano wa radio Tumaini ambayo haiombi michango?
4.kwanini hawatangazi matumizi kama walivyo hodari kuomba msaada?

Hii kuomba omba kila saa inakera kwa sababu unakuta mtu anataka kabda kusikiliza mafundisho au kwaya unakutana na kipundi cha michango tena cha lisaa lizima.
Jitafakarini kama hamjiwezi muwape wenye pesa wakiendeshe na sii kuomba kila saaa

Nakaribisha mawazo pia

Asanteni
 
TUMSIFU YESU KRISTO...!

Kweli baba padri John Maendeleo ebu sadifu kidogo jina lako..!

Mnahitaji kuajiri watu wabunifu wa kuibua miradi, michango inakera aisei kila saa ata huo uinjilishaji mtaufanya saa ngapi..! Tafuteni watu wabunifu kuwaibulie miradi ya kikanisa but inayolenga kuingiza kipato na uinjilishaji.

Hatuwezi kuchanga milele maana lazima kuna vitu vingine na kuanzishwa redio nyingine.

Fr. Maendeleo bila shaka umenisikia vyema.
 
Unajua siku hizi hakuna cha bure, kama unavutiwa na matangazo yao sharti uyalipie na namna pekee ya kuyalipia ni kuchangia kwa hiyari. Hawana matangazo ya biashara kwa hiyo muda huo hutangaza watu wanaowachangia. Kwenye TV ukilipa milioni moja wanakutangaza sawa tu na wao Maria ukichanga buku wanakutangaza kama unataka.
Unakwazika na maria wanapowatangaza wanaowachangia ,mbona haukereki na RFA au claud wanapopitisha matangazo kila SAA?
 
Milele amina nafikiri ni wakati wa kuwatafuta wahusika na kuwashauri ni wakati wa mapinduzi sasa hawawezi waajiri vijana creative
 
Chanzo cha mapato kwa radio yeyote ile ni matangazo ya biashara, kwa hiyo wakiaanza kufanya biashara hiyo , sizani kama watafanya kama lengo lao linavyowataka. Hakuna radio duniani ya kidini iliyofanikiwa nje ya fundraising toka kwa waamini wake.
Nazani pia radio maria coverage yake ni kubwa hivyo hata operating costs ni kubwa pia,
 
Mimi namshauri Padri Maendeleo kutanua coverage ya hii radio toka miji 13 hadi angalau miji 30 kama anataka mapato zaidi toka kwa waumini na wasikilizaji wake.
 
Kweli kabisa. Redio imekuwa rent seeking facility. Hadi usiku wa manane michango. Nja mbadala ya ku raise fedha inahitajika. Wakati mwingine inakuwa kero kuisikiliza.
 
Mleta mada hajui anachokitetea kama Mkatoliki..!!!!

Kama ni suala la michango ya kuitegemeza Radio Maria mbona hata Kanisa lenyewe linategemea mchango toka kwa waumini...???

Nakuhahakishia hivyo vitegauchumi vikiwepo,
NB;Matangazo ya biashara hivyo vipindi vya nyimbo za tafakari utazisikia kama unavyosikia sasa.

Na kabla ujarusha uzi kwanza ungechunguza the main concept ya Radio Maria,
Yani nikiwa na maana vipaumbele vyake alafu uviweke huku kisha tujadili.

Hebu jaribu kufanya hivyo kisha uje tena tujadili.

Asante.
 
Kuna siku nilisikia wamekusanya karibia million 400 sasa najiuliza kwanini wasizizungushe kwenye biashara yenye tija wakaachana na utegemezi imekua kama ni radio ya michango matangazo ya michango yamezidi mpaka lengo la radio.
 
Sio kwamba kila saa kuna matangazo ya michango, ni kwamba muda unaowasha redio yako kuisikiliza Radio Maria ndio unakuta ni kipindi cha michango. Vipindi vya kujenga roho vipo kila siku....
Tofautisha kauli mpendwa katika Kristo.
Hakuna mtu anaelazimishwa kutoa mchango. watu wanatoa kwa mapenzi yao. na wengi hutoa wakiwa na nia katika mioyo yao hivyo basi Radio ya Mama itaendelea kuchangiwa tuu!!!!!!!

Sauti ya kikristo rohoni mwako.
 
Ni kweli,
Wangebuni miradi ambayo itasaidia kuendesha kituo,
Wangeomba michango kama mtaji wa kuanzisha miradi ili baada ya miaka kadhaa wajitegemee
 
Hata mimi kwangu kero michango kila saa tena kila siku kila kipindi umasikini gani huu usioisha? Kwanini kisitengeneze mipango endelevu yakujitegemea?
 
Mimi namshauri Padri Maendeleo kutanua coverage ya hii radio toka miji 13 hadi angalau miji 30 kama anataka mapato zaidi toka kwa waumini na wasikilizaji wake.
Katiba ya tanzania inakataza kuongeza coverage kwa radio za kidin
 
Ivi wakiruhusu matangazo ya kibiashara,matangazo ya dume condom watapokea kweli?
 
Madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa Radio hiyo ni kuinjilisha na sio Radio ya kibiashara, hata unapoenda kuwachukua waje kwenye Parokia au Kigango chako ili warekodi Misa au wairushe live huwa hawakwambii kiwango, bali viongozi wa Kanisa ndio wanaamua wawalipe kiasi gani,
Ni Radio ambayo ina malengo taofauti na Radio kama Tumaini ambayo ni ya kibiashara

TUCHANGIE RADIO MARIA JAMANI,
 
Lengo hapa sio ku make profit..lengo ni kutengeneza kipato cha kuwezesha kujitegemeza..na ndio lengo la post
 
Hii ni sawa na kanisa liache kupokea sadaka na kuanza kujitegemea na miradi yake
 
Lengo hapa sio ku make profit..lengo ni kutengeneza kipato cha kuwezesha kujitegemeza..na ndio lengo la post

Ndio maana nikakwambia misingi ya kuanzishwa kwa Radio Maria sio ya kujiendesha yenyewe bali kiendeshwa na waamini wenye moyo safi, hilo unalosema la kutafuta kipato lipo nje ya misingi ya uanzishwaji wa Radio Maria Sauti ya Kikristo Nyumbani mwako
 
Lengo hapa sio ku make profit..lengo ni kutengeneza kipato cha kuwezesha kujitegemeza..na ndio lengo la post
Hivi huwa unatoa sadaka kanisani kweli..???
Nina mashaka na wewe...!!!hata kama utakuwa unatoa ni kishingo upande.

Acha tuichangie Radio Maria kwani inatoa elimu nzuri ya kikristo,inasaidia wale wasio jiweza kupata ibada ya misa takatifi wakiwa kitandani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…