Radio Producer
JF-Expert Member
- Feb 4, 2011
- 728
- 322
Ndugu yangu Radio Producer, juzi juzi ulikuja humu kwa utambulisho wa kitafuta kazi baada ya kuhitimu kozi ya Radio Producer.Salam wana JF,
Kwa wale wote wanaotaka kusoma Uandishi wa Habari, Utangazaji na Radio Production naomba uni PM ukieleza haya:-
1. Unaishi wapi?
2. Upo tayari kusoma kuanzia lini?
Nitakupa gharama zetu zote na utaratibu mzima. Tunataka kujua idadi ya wanafunzi wote! Asante.
Ndugu yangu Radio Producer, juzi juzi ulikuja humu kwa utambulisho wa kitafuta kazi baada ya kuhitimu kozi ya Radio Producer.
Tukakuelejeza sehemu za kuomba kazi lakini kutokana na elimu yako ya vyuo vya uchochoroni, hukujisumbua hata kutafuta hiyo kazi japo upate experiance.
Sasa leo ndio yamekuwa haya!? yaani ghafla umekuwa mwalimu?! au na wewe baada ya kihitimu uchochoroni sasa nawe umefungua uchochoro wako kutaka kuwalia watu pesa zao?!.
Kama wewe ni mkweli na sio tapeli naomba ueleze tuu hayo mafunzo mtayaendeshea wapi ili nijitolee kuwafanyia due diligence wana jf kabla hawajaingizwa mkenge.
Asalamu Alaykum mimi nataka hayo mafunzo lakini naona hakuna details zinazoeleza suala hilo naomba kufahamu kwa sababu nahitaji kujua yatachukua muda gani kwa sasa kuanzia mwezi wa agosti sitaweza kujiunga ikiwa kabla au baada basi nipo tayari ila mimi nipo zanzibar, hata hivyo natanguliza shukurani kwa dhati kabisa