Rafiki alivyotapeliwa kishirikina

Rafiki alivyotapeliwa kishirikina

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
1,503
Reaction score
2,426
Wasalaaam na wasalimu wakuu sio mwandshi mzuri makosa muyapotezee.

Twende kwenye kisa mwaka 2015 niliingia nchini msumbiji nilikwenda kwa rafik angu alikua anafanya kazi zake uko alikua na duka na ishu zingne, ila sehemu iyo ni mgodini uko sitaji sehem gani ila iz ni baazi ya sehem ambazo watu uhenda sana uko wapiga ponchi na wengne nami nilikua huko.

Turo, kagurue, sifuri d , mtepweshi n.k humu ndani wengne wanajua ayo maeneo. Hizi ishu zake za biashara zilikua zikiingiza pesa vizuri tu kwake.

Uyu rafiki tulisoma wote secondary form 1 to form 4 kudoji, kuibia wana kijiji kuku akizubaa tulipga sana.

Sasa ye akaingia msumbiji kitambo na mwaka huo 2015 Mi nilienda uko nikapiga mishe baada ya mwak a mmoja nikageuka ye aliendelea.

Mwaka wa 2017 alikuja town na ishu zake azikua vzuri sasa kule mambo ya ushirikina sio mchezo na rafik angu uyu na waganga ilikua ndio kimbilio lake, humwambii kitu.

Siku iyo alifika home tukapga story nyingi then mida akasepa alikua akai mbali sana na niliko mimi.

Usiku ule akanipigia oi mwanangu kuna bonge la mchongo asubuhi tuonane bila kukosa sawa? Nikamjbu poa. Kweli asubuhi akaniambia nipande pkpk niende alipo nikafika nikamkuta na kaanza maongezi. Akanipa simu yake chukua simu iyo soma meseji nikacheki meseji ilikua hivi:

MJUKUU WANGU-------akatajwa tajir mkubwa mkoani ruvuma wa mabasi na mkongwe ILE NDAGU IMEKUPA MAFANIKIO BASI ZAKO ZINA WATEJA NA BIASHARA YAKO INAKWENDA VIZURI NILETEE SHUKRANI NA SAIZ NNA DAWA ZA Congo UJE UONGEZE.

Ikaisha ivyo akaniuliza umeiyona hiyo text nikamwambia ndio we unasemaje rafiki, nikamwambia hazina hishu izi text zipo nying hapa mjini kwenye watu 10 hukosi watatu wenye meseji izi, akasema hapana uyu uhakika kampa utajir kumbe S----, halafu jana nilimpigia tukaanza kazi.

Nikamuuliza mkaanza kazi vipi?

Tayari nishampa pesa na tumeanza dawa alisema yupo Sumbawanga ningeweza kwenda ila sio shida kupitia simu angenifanyia nyungu za maana ntakua natuma pesa tu.

Mhm nikashtuka iyo pesa ya nini una mtumia akajbu ya kununulia dawa akaanza eleza iyo jana ilikuaje

Baada ya kumpigia akamwambia aende kwao ila njiani asiongee na mtu anunue udi akifika huko kwao achukue dishi akachote maji ya mtoni aweke ule udi ndani ya maji kisha aoge ila akumbuke kuto ongea na mtu yeyote yule akitoka aludi mjini akifika ndio amtumie pesa kiasi cha elfu 50 taslimu za Kitanzania.

Mshkaji akaenda kwao kwa mama ake mzaz kumbuka hapo toka atoke pori bado ajaenda kusalimia uko kwao alikua kwake aliko panga uko kwao pikipiki ni dakka 15 ivi ila alitakiwa aende kwa miguu ndio masherti na alifanya ivyo mateso makubwa,

Alifka kwao akamkuta bi mkubwa wake akala ndala tu na sura ya mbuzi akuna salamu wa chochote alicho ongea akachukua dishi akaenda teka maji na kurudi.

Akaoga na kusepa kurud mjini bila kuongea na mtu akawa ana elekea kutuma pesa apo ananisimulia ilivyokua jana yake bi mkubwa wake alitaharuki kuja yake na ondoka yake.

Njiani akakutana uso kwa uso na baba ake mkubwa, yani ile njo nije du masharti asiongee na mtu aisee alichoniambia hapa nilicheka vibaya mno.

Alisema uamuzi aliochukua ni kutoka nduki kali akampita baba ake shaaaaa ka mshale, alafu mbele kwa mbali akageuka kumcheki yule dingi aliona kaduwawa tu, hakujali kwa muda huo aliona utajiri upo njiani.

Akasepa mpaka kibanda cha M Pesa akamtumia yule mganga izo pesa huo ulikua mkasa wa Jana yake akinisimulia.

Nikamwambia ndugu utapotea hao matapeli jamaa aligoma, akasema uyu mkuu Mimi nins uhakika we subiri.

Mshkaji wangu ntapiga hela Mimi lazma nikutoe mwanangu tena ngoja nimpigie usikie ile kupiga akapokea alafu ana ongea sauti ya kilevi au ya mzee

Fanya kuongea apo alafu fananisha, mjukuu wangu kwema kwema babu umefikia wapi, nasubir tu pesa nikamilishe babu sio muda natumiwa.

Sawa kijana wangu saiz naelekea mlimani mizimuni nikazidi kuwaomba wakunga'arishie nyota yako utapata pesa nyingi. Sawa sawa babu, nimekuelewa. Akakata umeskia rafiki anavyosema Mi nikamwambia kama unasubiri utumiwe pesa kwajili ya ndagu izo pesa funga mzgo nenda pori uyu tapeli akuna kitu hapa Mi sikushauri kufanya ivyo ila kama unahamua kufanya ivyo wewe kama wewe basi sawa.

Jamaa akakazia usiwe na shaka Mi nafanikisha ili ghafla pesa ikaingia kwenye simu yake akasema nipeleke town yule mganga alimpa maagizo anunue kipande cha sanda, kuku mwekundu jogoo, wembe, kisu, jembe mshumaa ndoo jekundu, pamoja na begi ili la kuhifazia pesa zitakapoanza kutoka alafu aende mlimani porini awe peke ake akafanye alivyo muagiza ivyo akuniambia muda huo ila alifka sema badae uko mbeleni.

Basi tukachukua boda mpaka soko kuu tukadaka kuku, jembe na ndoo kisha shop tukachukua begi la kuwekea pesa zikianza kumwagka tukaenda maduka ya wahindi kwenda kuulizia sanda tukachukua kipande tu ila alilipa pesa ya robo wakuu hapa niliona aibu dhahiri, niliona hapa tunaonekana washirikina.

Aisee mambo aya bas tu tukakamilisha kila kitu fresh tuka toka hapo mbele kidogo mshkaji wangu sasa ndio alikiua anaenda kwenye mlima flani uko porin kuufwata utajiri nikampa neno.

Mwanangu isijekuwa uyu kuku unaenda kuchinja kumbe ni bi mkubwa au mwanao au ndugu tu.

Akasema usihofu kani hakikishia akuna kafara ya mtu basi akazama mfukoni akanipa buku kumi kisha akaenda uko porin Mi nikarudi
home

Njiani niliwaza sana hii ishu ila nikapata nguvu. Mi nilisha mkatalia ila huko kaenda kwa matakwa yake mwenyewe.

====

Tusonge. Basi mshkaji akaelekea kule msituni kwajili ya kwenda kufanya utundu na kukamilisha dawa na hatimae kupata utajiri kama ilivyo pangwa.

Maelezo haya alinambia baadae kwamba baada ya kufika uko porini, alichimba shimo kubwa lenye uwezo wa kuingia lile ndoo vizuri kabisa wakati huo vitu vingne pamoja na kuku viko chini, kisha akamchukua yule kuku kwajili ya kumchinja.

Akamuweka vizuri kumuelekeza kibra ghafla akaponyoka na kutimua nae akaanza kumfukuza bahati nzuri vile vichaka na miti miti vilifanya yule kuku asikimbie vizuri akafanikiwa kumshika na kurudi nae sehemu husika salama kabisa.

Basi akamchinja yule kuku na damu ya kuku akaielekeza kwenye lile shimo alafu akachukua wembe akajikata yeye kidoleni kisha zile damu zake akazichanganya na zile za kuku aiseee aya maisha mungu atuhurumie.

Kisha kile kipande cha sanda akakichukua na kumvirigia yule kuku mfu na kumtumbukiza kwenye lile ndoo na kulifunga hii alimaanisha kwamba jinsi yule kuku atakavyokua anaoza na kutoa funza au mabungu ndio pesa zitaanza kuja kwa kasi ya ajabu.

Halafu akamfukia pale kwenye lile shimo likiwa limezkwa yule kuku kama mtu maana na sanda juu sio mchezo. Alafu akachukua jembe na kuchimba shimo jingine pembeni na kuweka lile begi ambapo mtakua zikikaa zile pesa alichimba na kuweka lile begi na ndani ya begi aliweka ule mshumaa, huu mshumaa akuniambia ulikua wa kazi gani kazi ikawa imekwisha salama utajiri upo njiani.

Lile jembe na mabaki mengne kisu alimwambia akishamaliza avitupe uko uko porini na akuna mtu atakae vichukua zaidi mizimu itakuja na kuchukua zile zana na yeye aondoke akisubir aambiwe kwenda kuchukua pesa tu ndio kikicho bakia.

Akatoka ile anatoka tu kuna mtu akamuona kwa mbali anapita akalala chini asije yule mtu akamuona na ndagu yake kuharibika baada ya yule mtu kupotea zake nae akaondoka

Kwa makini sana nilikua nikimsikiliza uyu jamaa yangu na huo ujasiri wake, basi alivyotoka uko kama kawaida akaanza kuuchapa wa mguu mpaka nyumbani kwake masharti aliyopewa atakiwi kupanda usafir wowote atatumia miguu tu mpaka atakapoanza kupokea zile pesa hapa jamaa yangu alikua anapata mateso sio mchezo ulikua nenda kwa mguu rudi kwa mguu alafu ni mbali aisee.

Pia akamwambia akae stand by muda wowote kuanzia sasa atamwambia aende msituni kuchukua pesa maana mizimu imefurahi sana akamwambia muda ntakao kupigia simu iwe usiku asubuhi mchana au jioni itabidi uende pasipo kuogopa na pesa zako zitakua tayari ongera sana kijana kwa moyo wa ujasiri kama simba.

Mizimu ipo bega kwa bega na wewe na hakuna atakae gusa pesa yako kwa nia mbaya. Basi siku ya pili ndio alikuja home tukapga story mbili tatu na jamaa alionekana kuchoka sana kutoka na ile kwenda rudi alafu kwa mguu.

Jioni ivi tukatoka wote mpaka kwake tukamkuta shemeji na mwanae tukasalimiana na story zingne mida flani mi nikasepa home.

Saa saba na robo usiku simu yangu iliita na nilikua macho sikulala kwani nilibet sasa nilikua nacheki matokeo ya mechi live score simu ilikua ya uyu rafika angu nikapokea.

Mimi== hallo
Jamaa-- ndio mkuu ndio naenda hapa
Mimi==kakupigia simu
Jamaa--ndio kasema niende kule tayari
Mimi===sawa safari ya kheri ndugu
Jamaa-- asante nafikiri kesho tutaanza life jipya
Mimi===OK poa

Basi bana usiku ule wa saa saba aka elekea kule msituni aisee hapa niliogopa vipi jamaa akipigwa nondo usiku huu itakuaje? na kule anakoenda ni porini hii ishu mbona kama mchezo tu kwani uyu jamaa ashtuki mhmm nilijiuliza alafu apo anaenda kwa mguu mpaka kule aisee hizi hela unaweza kua na moyo wa ajabu sana tena wa kikatili.

Sikuwasilana nae tena mpaka asubuhi kulupokucha breki yake ya kwanza home alikuja asubuhi tu nikajua hapa live jamaa kabutua pesa ndio kaniwai fasta tufanye mipango nikatoka nje fasta nijue kulikoni.

Jamaa anasema alivyofika kule porini na kwenda kufungua lile begi ni 000000 amna kitu akataharuki na kukaa kwa uchovu na kuchoka moyoni aliuzika sana.

Mbona amna kitu na babu kamuamsha usiku pesa ishamwagika tayari hapo anaongea nami yupo hoi miguu imebuka vumbi tupu kwa kutembea na alikua kavaa sendo mim mhm ina maana pesa amna yeyote ile akajibu ndio.

Ikabidi ampigie yule babu kumuuliza nami nikiskliza
Babu--- ndio kiajana wangu mpendwa
Jamaa- babu sikufamikiwa kuona chochote ule usiku
Babu--- hapana kijana au umekosea dawa?
Jamaa-- kila kitu kilienda sawa babu
Babu- wakati unatoka kuna mtu ulimuaga si ndio ni nani uyo
Jamaa akamtaja mke wake
Babu-- kijana kijana kijana umefanya kosa kubwa na mizimu imekasrikika na kuondo zile pesa mke wako mwanzo ulimshirikisha?
Jamaa-- hapana babu
Babu--ndio kosa hilo na ndagu imearbika kijana ilitakiwa mke wako angejua toka mwanzo apo ungeondoka kimya kimya usingeaga kwake, na sasa inabidi tuanze upya sasa.
Jamaa-- lakin sikumwambia naenda wapi
Babu-- ukutakiwa kuaga kwa mkeo ikibidi kimya utoke bila kuaga.

Mhm niliguna moyoni hapa nikawaza uyu babu alimpigia simu jamaa usiku sana bila shaka alijua awezi kwenda mshkaji alienda na sasa kaleta kizingizio cha kuaga lakini pia kwenye kutuma pesa alimwambia asiongee na mtu bila shaka alijua endapo akiongea na mtu na kuingizia hili swala asingeenda kutuma na mpango ungefeli nikazidi kukazia mwanangu uyu mzee muongo.

Jamaa alibisha hapana mkuu Mimi hapa nimekosea masharti tu kama alivyosema inabidi tutengeneze dawa nyingine akuna namna yani mshikaji alimuamini uyu mtu 100%

Dakika chache babu akapga simu sasa itabidi tutengeneze ndagu mpya ile ya damu itabaki kule na itaungana na hii na sasa mahitaji ni haya

Apo kwenye mahitaji ndio nilichoka kabisa ikawa ivi:
Kijana anatakiwa ng'ombe mkubwa, mafuta ya simba na mafuta ya mahiti hii atakiwi kuchelewesha inabidi tuwai iungane na ile ya kuku tukamilishe tafuta ivi vitu haraka iwezekanavyo tufanikishe jambo hili mizimu inasuburi kuziachia zile pesa sawa, jamaa akajbu sawa mzee akakata simu.

Mhm niliguna nikavuta pumzi na kuziacha nikamwambia kwa mahitaji ayo ndugu kwa ela ipi Mi sina uhakika na hili jambo mwana stuka mshkaji akasema no nipo hatua ya mwisho yanipasa kutkeleza, nikamwambia mwanangu mafuta ya simba mafuta ya mahiti wapi yanapatika, tutapata wapi na tutamuuliza nani si tutaonekana wachawi ndugu tena sisi vijana hivi majunk tu na ushirikina mbona watu watatushangaa kuulizia vitu ivi acha izo kuhusu ng'ombe uku kusini ng'ombe mkubwa milioni mpaka laki saba mwana mbona pesa nyingi ivi? Pesa ipo alijbu ntawacheki jamaa wanitumie mhm pesa ya kwake sio shida niliwaza ivyo nikamwambia basi poa ayo mafuta ya simba na mafuta ya mahti akasema ngoja nimpigie babu nijue tuanafanyeje.

Akapiga na kumuelekeza ishu nzima ugumu wa kupata ayo mafuta na ukali wa bei ya ng'ombe majibu yakawa ivi
Mjukuu uku kwetu ng'ombe bei rahisi tu na ayo mafuta usijali utatuma pesa ya ng'ombe laki tano tu anaptikana namfanyia dawa huku pia laki tatu ya mafuta ya simba na laki na ishrini mafuta ya mahiti ivyo vitu nyote ntavipata kwa mda mchache tu na kukamilisha.

sawa babu nipe kama saa moja ntakua nakamilisha iyo pesa alijibu mshkaji wangu aisee hapa sikua na neno simu ilikatwa tukapiga story za hapa na pale.

Akapigiwa simu toka porini hapa akaingiza ili swala kwa kuhitaji pesa toka kwa mfanya kazi wake jumla ilikua laki 9 na elfu ishirini inahitajika akamwambia dogo---- nilushie milioni mpesa Nina shida nayo fasta usikawie dogo akufanya ajizi akaenda dukani na kutuma mzigo dakika chache pesa ikaingia na akanipa Mimi niitume ile pesa inyo itajika kwa yule babu kama ilivyo na ya kutolea asipate shida yule babu.

Wakuu itasonga

Jibu la kule juu JamiiForum na teregram sio ndugu Bali majina tu yanafanana chaooooooo
 
Kastory kazuri kuliko zile za Shigongo, na mm nazipata sana hizo sms
ila kweli usitupeleke Telegram km @Lwande Magere
 
Baadae na wewe utatuhamishia telegram na kutaka buku?
 
Huko mbali mi nilipigwa na yule wa Jf alijiiita Simba nini sijui wa Tanga[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Niseme tu mod wame onganisha Uzi kipande cha pili kipo apo juu
 
Back
Top Bottom