Kuna rafiki yangu tunamesoma naye. ameniomba ushauri afanye nini baada ya kugundua kuwa rafiki yake wanaefanya naye kazi anatembea na mpenzi wake. Huyo jamaa anajua kila kitu kuwa huyo ni demu wake na huwa anamwelezea kila kitu kuhusu migogoro yao naye jamaa huwa anampa ushauri mwingi sana. Lakini amekuja kugundua kumbe huyo rafiki yake anatembea na kipenzi chake. sasa akaniuliza afanye nn maana jamaa wanafanya kazi ofsi moja.
Mwachie huyo dame hakufai(ni ndimalakuwili). Mjulishe rafiki yako kuwa umeshajuwa janja yake na kuwa umemwachia dame. Hata akikataa baada ya kumpa ushahidi nae pia achana nae. Rafiki kama huyo si mzuri. Ukiendelea naye anaweza kuku umiza hata nyumbani.
Rafiki na Mpenzi, kupoteza vyote kwa wakati mmoja ni pigo kubwa sana! Lakini nafsi yake inapaswa kumuungoza, moyo wake itamuonyesha uchungu upi ataweza kuubeba!
Inaelekea na yeye sio mwanamme mwenye maamuzi yakiume,kwanza huyo si mchumba wala si mke, Kama amepoteza mahari au pesa za harusi, kama wamependana na Huyo rafiki yake wa kazini amuachie kwa Amani tu,yeye atafute mwengine mbona wamejaa tele wazuri wa sura na tabia! Huyo paka mapepe aachane nae...
Aidha amsamehe au akubali kuendelea kuwa BF mweza, ila ili kupunguza machungu mwambie na yeye atafute mnyonge ammegee. Ndo matokeo ya kuanza kumweleza rafikio maswala ya mpenzio anaanza ku-test zali.
Kwanini mmemchukulia kana kwamba huyo dada hajitambui? Hivi watu wakitoka mpaka wakalalani kuna sehemu kuna alama inaonesha nani alimuanza mwenzie? Na hata kama hio alama ingalikuwepo kwani kabakwa? NO! (usha sema anatembea nae, that means more than once); Haya basi anataka amchukie rafikiye mpaka anafikiria la kumfanya/kufanya - Are you saying bado karidhia kuendelea na huyo mdada? Haya mambo ukiaendekeza utaendeshwa saana..... Always mwanadamu ana kutreat the way you want/let them be.
Mpe pole saana kwa yalomkuta na kutojua/tambua kua hao wawili woote si wema kwake. Na nampongeza bado anam consider kua eti "mpenzi wangu" aaarrrgh!! I am SO fade up of this lousy game!!