Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
RAFIKI NI ADUI ALIYE KARIBU
Na, Robert Heriel
Rafiki ni mtu ambaye unaukaribu naye wa kimahusiano, unayeshirikiana naye katika mambo mengi, unayemuamini, unayetunziana naye siri na kusaidiana katika shida na raha.
Moja ya kanuni kuu ya ulimwengu. (Universal law) ni ''kutomuamini mtu yeyote'' (Trust no one) Kama alivyosema mwanafalsafa Niccolò Machiavelli mwenye asili ya kiitaliano katika Principle of management and Adminstration.
Machiavelli (tamka Makyeveli) katika falsafa za kisiasa(political philosophies) alitoa kanuni nyingi sana ambazo viongozi wengi wakubwa na mashuhuri duniani wamekuwa wakizitumia katika shughuli zao za utawala.
Miongoni mwa falsafa zake ni pamoja na hizi;
1. "Kamwe usimzidi kiongozi/boss wako" (1. Never Outshine the Master)
Yaani unapokuwa na kiongozi wako hakikisha hata kama unauwezo, ujuzi au elimu zaidi yako usionyeshe mbele yake usije ukapata sifa zaidi yake. Hii itakuweka sehemu mbaya.
2."Uliza/Jifanye kama Rafiki, Fanya kama Jasusi/mpelelezi" (Pose as a Friend, Work as a Spy)
Tafuta taarifa kwa mazungumzo ya kirafiki ili kujua dhamira au mipango ya watu, kuwa mpelelezi au jasusi, kwa kupata taarifa kwa huo ndio ulinzi wako.
3. Muangamize kabisa adui yako (Crush your Enemy Totally)
Unapopigana na adui yako usimpige nusu nusu mpige mpaka umuangamize kabisa. Usipofanya hivyo utasababisha Revenge isiyo na ulazima.
4. Jua ni nani unayeshughulika/ pambana naye, Usifanye kwa mtu asiyehusika (Know Who You’re Dealing with – Do Not Offend the Wrong Person) Hakikisha unayepambana naye ndiye adui halisi, usijepambana na mtu asiyehusika, kumbe adui yupo pembeni.
5. Usijitolee kwa ajili ya mtu yeyote (Do Not Commit to Anyone)
Dumisha uhuru wako, usijitolee kupambania wengine, bali wafanye wapambane wenyewe, hii itawafanya wakuone wewe ndiye mkombozi.
6. Kamwe usiwaamini sana Marafiki, Jifunze jinsi ya kutumia Maadui ( Never put too Much Trust in Friends, Learn how to use Enemies)
Jamani naomba niishie hapa kwa habari za huyu Niccolo Machiavele na falsafa zake, ingawaje zipo nyingi sana lakini lengo langu sio kuzielezea bali kutoa mifano michache, kisha nieleleze suala la kutokumuamini Mtu yeyote yule.
Watu wote waliofanikiwa katika utawala na wenye mafanikio makubwa duniani walifuata au walitumia baadhi ya kanuni hizo hapo juu.
Rafiki ni watu wazuri sana ikiwa tuu hutavunja kanuni ya msingi ya Trust no one(usimwamini yeyote). Rafiki anakuwa mbaya pale unapoanza kumuamini. Unapomuamini rafiki yako ndio unaanza kumfanya adui yako wa karibu.
Watu wote wanaolia kwa uchungu katika matatizo yao chanzo huwa ni marafiki au watu wao wa karibu. Ni kosa la kiufundi kumuamini mtu, kumpa siri zako hasa zile siri ambazo ni nguzo za maisha yako.
Huweza mpa rafiki yako siri ya mafanikio yako, hii ni kwa sababu 99% ya roho ya binadamu imejawa na ubinafsi na wivu. Kitendo cha kumwambia siri ya mafanikio yako ni kuamsha hisia za wivu juu yako, na huo ndio mwanzo wa kuanguka kwako.
Visa kama Samson na Deila hutufundisha hayo, kuwa Samson awali alikaza sana kutokumuamini Rafiki yake wa kimapenzi aitwaye Delilah. Lakini baada ya kushawishi sana yaani Delilah kutumia kanuni isemayo ""Uliza/Jifanye kama Rafiki, Fanya kama Jasusi/mpelelezi" ( Pose as a Friend, Work as a Spy)" Ambayo nimeitaja hapo juu, Samson akakubali kutoa siri akijua Delilah ni rafiki mwema kumbe ni adui aliyekaribu. Hakuna asiyejua kilichotokea.
Kisa cha Sadam Hussein hakuna asiyejua jinsi ilivyotokea mpaka akaja kukamatwa na kuuawa.
Kisa cha Yesu na Yuda Msaliti ambaye alikuwa rafiki yake.
Kwenye Ulimwengu huu, tahadhari ni muhimu sana kwa kila hatua unayopiga, kila hatua inaweza kuwa na mtego. Unapokanya ni lazima uhakikishe ni salama, wanaokuzunguka lazima uwatathimini, lazima uwajue kama kanuni isemayo "Jua ni nani unayeshughulika/ pambana naye, Usifanye kwa mtu asiyehusika ( Know Who You’re Dealing with – Do Not Offend the Wrong Person)"
Ukitaka kufanikiwa njia rahisi ni kujua kuwatumia maadui kuliko kuwatumia marafiki. Adui yupo real, Rafiki mara nyingi huwa wanafiki. Ni heri umuamini adui kwa maana unamjua.
Yesu wa Nazareth(Mwanafalsafa anayenikosa) aliwahi kusema adui wa mtu ni yule wa karibu. Na hata wahenga walisema kikulacho kinguoni mwako. Misemo hii ni king'ora kwetu kuwa lazima tuchukue tahadhari tuwapo na Rafiki zetu.
Rafiki wa kwanza ni Mke wako/ mume wako japo wengine wanaweza kukataa lakini huwezi kuwa na mwenzi ambaye sio rafiki yako hiyo ni ngumu. Usimuamini sana mke/mume wako mpaka utakapofikia kiwango cha juu na muda ukiwa umeyoyoma sana kiasi kwamba hata akifanya shambulizi lolote litakuwa halina madhara makubwa.
Marafiki wengine huweza kuwa wazazi, ndugu, jamaa na wengineo.
Muhimu kuzingatia. Usiwe na marafiki wengi kwani kwa kufanya hivyo hutaweza kuwa-manage hivyo unajitengenezea mazingira ya kuzungukwa na adui wengi.
Pili usimuamini yeyote yule.
Kama ukiambiwa utaje rafiki zako mpaka wafike kumi nakushauri fanya hivi
1. Mungu
2. wewe
3. wewe
4. wewe
5, 6, 7, 8, 9, 10 zote wewee.
Hiyo ni Universal Law kuivunja hiyo ni kujitafutia matatizo mwenyewe.
Mungu anasemaje kuhusiana na hili?
Mungu anasema; Usimwamini mtu yeyote zaidi yake. Imani huleta mategemeo. Na Mungu anasema; Ole wake amtegemeaye(amwaminiye) mwanadamu.
Kumuamini mtu ni kumtajarajia kwa mambo fulani. Matarajio ndio huumiza watu. Ulimuamini mtu hawezi kukusaliti sasa amaekusaliti, moyo unakuuma.
Hakuna amri inayotaka watu waaminiane hasa amri ya za Mungu. Bali ipo Amri moja tuu, Mpende jirani yako kama nafasi yako ilivyo.
Kosa kubwa linalofanywa na wengi ni kuchanganya Upendo na Imani ambapo kimsingi ni vitu viwili tofauti licha ya kuwa vinaweza kushirikiana.
Kutokumuamini mtu kutakufanya uishi kwa tahadhari, pia kutakufanya usiumie kipumbavu na kizembe.
Sheria hii ni muhimu kwenye kila nyanja ya maisha. hasa kwenye Utawala na mamlaka, Biashara, makazini, na ndani ya ndoa.
Kumbuka; Penye chuki wema Ulitangulia.
Kwa leo niishie hapa, maana wadau wangu hawaishi kulia makala ndefu.
Barikiweni!!!!
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dodoma