Rafiki niliyemuamini akanipora mchumba, Mungu akanilipia!

Hili darasa tosho inatakiwa usimuamini mtu kupita kiasi kuwe na mipaka.
:spy:
 
Dah,pole kwa mkasa,ila hiyo heading nadhani wange_edit,haiko sawa
 


Yote umenena....My take:
Ukiona kitu hakiwi kama kilivyotarajiwa jua kuna kitu unaepushwa nacho...
 
Ama kweli ubinadamu kazi na fadhila mfadhili mbuzi maana utakunywa mchuzi
 

nice story......................inafundisha pia
 
Tamthiliya sijui au Riwaya si mbaya lakini huyu msichana kaamuwa kusuta jigijigi? Naona hakupata tena mpenzi au vipi?
 
Dah!very sad story!!hiyo ndo mitihani ya maisha!

hiv manifestation ndani ya mwaka mmoja mpaka kufa? Hata mtoto mdogo ambaye immunity yake si nzuri haiwagi hivyo!! Hii ni kama muvi za kina kanumba tunazoziangalia bahati mbaya tukiwa safarini kwenye mabasi ambazo unakuta shamba boy ana wave na raba ya 40000. Muwe mnaulizia wajuzi hata kusoma around kidogo mkijua hata medical personel wanasoma. Huu ni uvivu na kutegeana kazi, tubadilike jamani.
 
Yani leo niko very busy na kama si kuwa wewe ni mwandishi mahiri nisingesoma habari yote hii bila hata kuruka mstari. Hivyo naomba nikusifu kuwa una kipaji cha kuandika... Ni watu wachache sana wenye uwezo kama wako wa kumvutia msomaji aendeleee kusoma tuuuuuu. Hongera sana.

Hiki kisa kinafaa kitungiwe kitabu... ni funzo kwa wanawake wanaovamia mapenzi ya watu na wanaume wanaoshobokea madada zao.

Mungu ni mwingi wa Rehema.. nina imani huyo dada atapata tu wa kuishi nae kama mume halali.

Ila haya mambo jamani yapo... Mimi ndio maana nimeshajiwekea hakuna cha udada na ukaka simply bcoz mmetoka mkoa mmoja... Nasikia watu wanamegana sana in the name of Kaka... Dada

Kuna mwananmke mmoja ana shepu utadhani amechongwa alianzaga kujipendekeza kwa mume wangu eti dada nikasema dada my foot. Ni rafiki wa first cousins wa mume wangu... Eti anakuja home wifi niliuchuna mpaka kaingia mitini.. Fa mchezoo.
 
mmhh!! 41yrs with no kid?
Hii inamaanisha nini, alikata tamaa?, akutongozwa tena?, ana matatitzo ya kizazi au ali-abstain completely.
 
Ndugu huwezi jua ukimwi umeingia lini kwenye mwili hasa kama hufanyi check ups. Inawezekana ameugua mwaka mmoja lakini kaukwaa 5 years a go. Achana na hili gonjwa halina formular. Wengi wanakufa vibaya kwa kukataa ukweli...au kwa sababu ya kuzaa... au walikuwa na magonjwa mengine ya kudumu kwa maana kuwa ni wadhaifu kabla ya kuukwaa

 
Huyu atakuwa alikatishwa tamaa na akakosa imani na mapenzi au kupenda na kupendwa tena. Inataka moyo wa chuma kurudi kuwa normal baada ya kufanyiwa kitu kama hiki... wengi wanapoteza hata mvuto kwa frustration. Na ukikosa trust huwezi kupenda.


mmhh!! 41yrs with no kid?
Hii inamaanisha nini, alikata tamaa?, akutongozwa tena?, ana matatitzo ya kizazi au ali-abstain completely.
 
[h=2]'Mungu akanilipia!' mbona kwa kauli hii inadhihisha wazi kwanba dada huyu alikuwa bado na kinyongo na anafurahia matokeo ya vivo vya wawili hao.[/h]
 
Dada,pole sana.Usihofu maisha yanaweza kukamilika hata bila mume au bila watoto kama utajikubali,lakini ume imara.Kuhusu mahusiano,ni kweli wanaume tuna matatizo mengi sana as well as wanawake,but jifunze kuwa na mtazamo chanya.Inawezekana ukawa na wakati mgumu sana lakini utashinda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…