Rafiki wa Mashali aeleza alichozungumza na Mashali wakati yupo hospitali

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Rafiki wa karibu wa marehemu Thomas Mashali
aliyejitambulisha kwa jina la Ally amesimulia mkasa
mzima wa kifo cha rafiki yake huyo. Ally alisimulia mkasa wa rafiki yake huyo akiwa msibani maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam,

Ambapo amedai kuwa juzi usiku alipata taarifa za
kushambuliwa kwa Mashali na watu wasifahamika
maeneo ya Kimara jijini humo. “Ilikuwa usiku nimekaa nyumbani Manzese
Madizini akaja dereva bodaboda anaitwa Yusuf
Kidevu akaniambia babaako wanampiga huko
Kimara wanamuua kama vipi nenda.”

“Nikahisi ni uongo kwasababu wakati mwingine
wanazusha tu, mara kidogo akaja mtu wa pili
akasema babaako anakufa huko Kimara,
kwa sababu alikuwa ni mtu wa pili kuniambia
nikaona bora niende.” “Nikaenda hadi Kimara, kufika pale nikakuta
wameshampiga wamemuumiza askari
wanampakia kwenye gari.

Nikalifata gari hadi Sinza, akapata kitanda akalazwa nikaenda
kumsalimia lakini saui ilikuwa inatoka kwa mbali
hadi usogeze sikio ndio unaweza kumsikia.” “Nikamuuliza imekuwaje, akasema kuna dereva bodaboda alimkodi lakini walivyofika Kimara
akampa hela kidogo wakaanza kuzozana ndio
mkasa ulipoanzia.”

“Alimpa shilingi 2000 lakini dereva bodaboda
alikuwa anataka shilingi 3000, akaanza
kumtukana Mashali akaona anadharauliwa
akampiga ngumi yule dereba bodaboda
akaanguka chini, baada ya hapo akaanza kupiga
kelele za mwizi wakaja watu wengine watatu wakataka kumpiga akapambana nao akawapiga.”

“Baada ya kuona wote hawamuwezi wote
wakaanza kupiga kelele za kumuita mwizi,
wakaongezeka watu wengine wakaanza
kumshambulia.” Mwili wa Thomas Mashali unatarajiwa kuzikwa
Jumatano jijini Dar es salaam.


Source: Shaffih Dauda
 
sasa na yeye ngumi kila mahali?tujifunze japo alikosea kumuitia mwizi.rip
 
Tujifunze kujishusha na si ubabe kwa kila jambo.
 
Uongo...
Aseme ukweli uliomuua mwenzie...
Walimsingizia Scorpion mbaya kumbe Said ndio Jizi linalofadhili mijizi na mtandao wao.
Kila muovu kwa sasa nguvu ya Umma itamuumbua. Vyombo vya Dola viendelee kuwalinda na kufaidika nao tu
 
Kweli viroba vinapunguza nguvu za asili yaani mtu 5 wamemkimbia mtu mmoja!!! Hadi wamemwitia mwizi!!!daa r.i.p kalale pahali pema bondia!![emoji86] [emoji86]
 
Kama walipatana kabla ya safari alifanya vibaya kudhulumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…