Rafiki yangu akifanya tiba za kienyeji hafanikiwi huku wengine wakifanikiwa kwa haohao wataalam

Rafiki yangu akifanya tiba za kienyeji hafanikiwi huku wengine wakifanikiwa kwa haohao wataalam

Black_Panty

New Member
Joined
Jul 18, 2023
Posts
2
Reaction score
4
Habr za muda, wataalam mlioko hap naomb ufafanuzi.

Kuna rafki yangu kila akienda kushughulikiwa swala la nyota, kutoa vifungo nuksi mikosi, kutoa jini mahaba ila hafanikishi, au akifunguka nkidogo tu baasi. Lakin akielekeza marafiki zake sehemu yeyote amekwenda wao wanafanikisha na wanapata wepesi kwa mambo yao.

Tiba amefanya Kwa wataalam tofauti wa vitabu, mizimu, kienyeji(Asili), tunguli, ata wa majini. Kaogeshwa Njia panda, Kwa kichuguu, kupigwa nyungu, Yaani kila mtu na mbinu yake lakini hapati wepesi inavofaa. Tambiko pia amefanya zaidi ya mara tatu lakini hamna.

Kaniambia nimpostie sabab haelewi mbona hapati wepesi kwenye Riziki zake....nyie wataalam ebu mtoeni maoni tujue tatizo lipo wapi. Mbona tiba za aina zote zinagoma kwake na Kwa wengine zinatiki🤔
 
kwa hiyo wewe umefanikiwa kwa mujibu wa rafiki yako? kama siyo unaona wivu mafanikio yake kwa kuwa mganga wenu ni mmoja.
 
Tiba amefanya Kwa wataalam tofauti wa vitabu, mizimu, kienyeji(Asili), tunguli, ata wa majini. Kaogeshwa Njia panda, Kwa kichuguu, kupigwa nyungu, Yaani kila mtu na mbinu yake lakini hapati wepesi inavofaa. Tambiko pia amefanya zaidi ya mara tatu lakini hamna.!!!!

Kuna kitu kibaigwa usugu wa sawa kutokana na kukosa tiba sahihi Huku ugonjwa halisi ukiendelea kukutesa na kukuumiza.. Niliwahi kukutana na hiyo changamoto! Nikatibiwa hospital kama 5 tofauti kwa muda wa miezi mitatu kumbe nilikuwa natibiwa magonjwa ambayo nilikuwa siumwi[emoji35]

Sasa kwenye tiba za kienyeji hali ndio mbaya zaidi kwakuwa inaumiza mwili, inaumiza ufahamu na inaumiza ustawi wa kiroho

1. Mwili unaathirika kutokana na maumivu ya kuchanjwachanjwa kila wakati na kuachiwa makovu.
. Mwili unaathirika kutokana kupewa madawa yasiyo na vipimo vya maabara na kuchuja sumu.. Hivyo unazichosha figo na madini yako
. Mwili unaathirika kutokana na uchovu, kutokula vizuri, wasiwasi, kuamshwa usiku mwing, nknk

2. Kuumiza ufahamu.. Unapewa masharti ambayo kwa hali ya kawaida usingeweza kuyafanya
. Dhana ya kuona unazidi kupoteza muda na pesa lakini hufanikiwi utajayo
. Msongo wa mawazo nknk

3. Ustawi wa kiroho
. tiba za asili kwa akili ya hayo mambo huwa zinashughulika na roho zaidi.. Binadamu huwa ni msafi kiroho bila kujali dhambi zake mpaka pale anapoingia kwenye hizo mishe
. Tiba yoyote wenye kujihusisha na ushirikina hiyo ni madhabahu ya roho.. Hivyo kila unapobadili mtaalam unajenga madhabahu mpya rohoni mwako.. Kwahiyo baada ya muda badala ya zile tiba kukusaidia, kinajitokeza kitu kipya.. Mapigano ya kiroho kugombea umiliki wa mwili wako.. Manake mwili wako ndio makazi yao. Hapo unadhani kuna kupona?
. Tiba zinatofautiana nguvu kuna nyingine hutibu haraka na nyingine huchelewa kutokana na nguvu ya kiroho ya mtu hivyo hupaswi kuhangaika Huku na kule
. Kuna miili na kuna roho zina mzio mkubwa na wavamizi.. Hivyo unapotumia hizo tiba unaleta kitu kipya kisichotakiwa na wenyeji.. Kiasili miili na roho zetu vina nguvu za asili za kuweza kupambana na kushinda bila msaada wa maroho mengine..

Mwisho ogopeni sana shuhuda za watu kwenye hayo mambo .. Ukiachilia mbali madalali kuna wengine hushuhudia bila ithibati na wengine ni promo tuu..

Huyo ndugu kwasasa mwili wake umechafuliwa na kila aina ya tiba.. Kila mtu ana kipimo chake katikati maisha ..hatufanani kamwe hivyo asijilinganishe na wengine..atakufa kwa mawazo
Achukue muda kuutakasa mwili na roho yake.. Avipumzishe hivi viwili vifanye kazi kwa msaada wa chumvi.. Ili yale maroho yafunge virago yaondoke MOJA baada ya lingine mpaka atakasike asafishike kabisa kisha ataona matokeo..[emoji1545]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nikienda kanisani mambo yanazidi kua magumu wenzangu wakienda vitu vinanyooka.

Nitaenda kwa waganga wanne kama case study na kurudisha majibu.
 
Habr za muda, wataalam mlioko hap naomb ufafanuzi.

Kuna rafki yangu kila akienda kushughulikiwa swala la nyota, kutoa vifungo nuksi mikosi, kutoa jini mahaba ila hafanikishi, au akifunguka nkidogo tu baasi. Lakin akielekeza marafiki zake sehemu yeyote amekwenda wao wanafanikisha na wanapata wepesi kwa mambo yao.

Tiba amefanya Kwa wataalam tofauti wa vitabu, mizimu, kienyeji(Asili), tunguli, ata wa majini. Kaogeshwa Njia panda, Kwa kichuguu, kupigwa nyungu, Yaani kila mtu na mbinu yake lakini hapati wepesi inavofaa. Tambiko pia amefanya zaidi ya mara tatu lakini hamna.

Kaniambia nimpostie sabab haelewi mbona hapati wepesi kwenye Riziki zake....nyie wataalam ebu mtoeni maoni tujue tatizo lipo wapi. Mbona tiba za aina zote zinagoma kwake na Kwa wengine zinatiki[emoji848]
Umeeleweka mkuu(japo tatizo linakuhusu mwenyewe wala sio rafiki yako)
Anyway ngoja waje
 
Huyo ni kipenzi cha Mungu, Mungu hataki kumpeleka motoni Kwa dhambi ya shirki.....
Dawa aamke kila siku saa Tisa usiku, Kwa Imani yake aongee na Mola wake....pia atoe sadaka ya Siri.
Nakubaliana na ushauri wako, aufuate utamsaidia.
 
Huyo ni kipenzi cha Mungu, Mungu hataki kumpeleka motoni Kwa dhambi ya shirki.....
Dawa aamke kila siku saa Tisa usiku, Kwa Imani yake aongee na Mola wake....pia atoe sadaka ya Siri.
Uko sahihi kabisa Mimi nimeliona hilo yaani huyo akimgeukia Mungu mazima bila kupinda kushoto wala kulia aisee mtashangaa atakavyofanikiwa

Hapo upande Wa Mungu unamuhitaji hivyo hizo nguvu za Giza haziwezi leta matokeo maana tayari kunamamlaka kuu zaidi imeshafanya booking hapo

Ni swala la Muda tu na ameachwa ahangaike ili akitoka hapo abaki na njia moja tu yaani Kwenye mamlaka ya Nuru so anaandaliwa asiwe Mwenye kugeuka geuka
 
Ndege wafananao...ulipoenda ww hajafanikiwa pia? Isije kuwa shida ya kupata mume
 
Mi nikienda kanisani mambo yanazidi kua magumu wenzangu wakienda vitu vinanyooka.

Nitaenda kwa waganga wanne kama case study na kurudisha majibu.
Hahahahahah unaenda kujaribu Mungu sio mtu umtumie tu kufanikiwa afu usepe yeye huchunguza nia ya moyo

Nakupa mbinu hii iliyonisaidia amua sasa kuwa Mungu anijibu nitaendelea kumwabudu na hata asipo jibu bado sitaacha kumwabudu

Mambo ya mepesii au yazidi kuwa magumu sitaacha kumwabudu imradi Niko hai Basi Mimi na Mungu tu

Na ukishaamua hivi anza kuishi ulichokusudia

Itachukuwa muda kupokea unachotaka mpaka ibada kwako inengeke iwe tabia ndio matokeo utaanza kuyaona

Maana ikishakuwa tabia hata ukipewa unachotaka hautaacha ibada maana imekuwa tabia

Na Kwa uhalisia ibada mpaka iwe tabia inaweza chukua hata zaidi ya mwaka

Na ili ufanikiwe kujenga tabia hiyo Kwa haraka anza kuamka asubuhi Fanya ibada saa nzima mchana hakikisha unapata muda Wa ibada walau nusu saa na jioni hakikisha unapata walau saa au nusu saa ya ibada

Tenga siku moja katika week ya mfungo zingatia ratiba kuwa na nidhamu katika hayo

Usikose ibada za pamoja aisee na kuapia baada ya Muda hautakuwa ulivyo

Ukiona peke yako linakuwa gumu nitafute nikusaidie
 
Back
Top Bottom