Rafiki yangu akisikia mziki anaoupenda anaucheza bila kujali eneo, je ni pepo?

Jamaa sio mnafiki, anafanya ile mwili wake unataka na si kuangalia binadamu wa pembeni.Sio kwamba wewe hutaki kucheza ukisikia kamuziki unakokapenda ila kinachokufanya usicheze ni ile watanionaje.
Ni kweli lakini inakuwa kama utoto sasa,
 
Bora yy ana open hisia zake anywhere any time ,kuliko ukawa unataman kitu alafu una ogopa watu watasemaje...
kuna vitu vingine kujisitiri ni muhimu, unaweza ukawa na uwezo wa kupiga sahani tatu lakini inabidi ujivunge kidogo kwenye baadhi ya matukio ili usionekane mlafi
 

Ni tiba ya Kisaikolojia Kwake kutokana na yanayomsibu Kichwani ( Ubongoni ) Kwake.

Tena Shukuru akiwa anasikia Nyimbo azipendazo anafurahia na Kuzicheza kwani hizo nyingi angeweza hata Kufanya Jambo baya na msingsamini.

Tatizo la Kisaikolojia ni Kubwa Tanzania.
 
Ulevi ni ulevi. Tumbaku haramu,pombe,ulafi,uzinifu,kupiga chabo,mwizi,nk. Huo nao ni ulevi kupenda kuliko vuka kiwango.
 
Mimi nilitikisa kichwa ukweni,nilipoisikia nyimbo ya Diamond jeje,kumbe mamkwe ananichora tu

Kukutanisha macho,akatabasamu na kuinuka lile eneo,nikajawa na aibu kutwa nzima

Ilaaniwe K vant na ukoo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu nipo nae karibu hapa ninemsikia anataka kuanzisha bendi anatafuta wacheza shoo nataka nimuoneshe uzi wako ila nasitasita
 
Huyo ananifaa kabisa kuwa rafiki yangu. Huyo ni yeye kabisa na anajikubali, anajiamini na ni mtu mwenye amani sana na asiye na vinyongo wala hasira hasira hata ukimuudhi hana hasira za kutisha huyo. Hakika unarafiki mzuri mno.

Huyo Yuko vizuri na ninamoongeza, mwambie namsalimia na asije acha kupenda mziki na kuucheza. Mziki ni Maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…