Mkunazi Njiwa
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 8,538
- 7,559
Kule Kinondoni kulitokea ubishi mkuu wa kutunishiana misuli kati ya Meya kamarada mh.Songoro Mnyonge(diwani kata ya Kinondoni kama sikosei) na aliyekuwa DED wa Kinondoni mh.Sipora Pangani.
Zogo lile lilikuwa kubwa huku kila mtu akitumia ubabe wa "KITI" chake.
Nimekumbushia kisa hiki ili tupate "mawaidha" kuwa MOTO unaowaka katika MABARAZA YA MADIWANI NI MKUBWA kuliko huko BUNGENI.
Ukiacha ile kauli iliyotolewa bungeni ya "TUMBIRI" "iliyotrend" sana kati ya Prof.Muhongo na mkurugenzi wa sasa wa PPP kamarada mtunduizi msukuma wa Kigoma kamishna David Kafulila,baraza la madiwani linabaki kuwa "Kivu ya kaskazini" ya maneno. Nimeambiwa na madiwani wengi kuwa humo KAULI ZA KISHUJAA ndio "mwake".
Humo kedi ,zodo,masimango,kauli chafu ,kupotezeana malengo na muda kwa siasa za majitaka(tarnishing of image) ndiko "epicentre".
Ni kwanini hali iko hivyo?
Sisemi kwa ubaya ila wengi wasio na elimu kubwa utawakuta ndani yake zaidi ya BUNGENI.
Katiba yetu ya JMT inaruhusu "kujua kusoma na kuandika" kama MKONGOJO wa KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA ,basi wale wachaguliwa wengi wa kutetewa na KATIBA utawakuta humo BARAZANI [emoji1787][emoji1787]
Nimewafanyia kampeni wagombea udiwani wengi....najua ninachokisema....kati yao nadiriki kusema ni mmoja tu ambaye alikuwa na kiwango cha elimu ya UZAMILI na sasa ni MKUBWA huko TRA....[emoji1787]
Huyu BWANA nilikutana naye nikiwa kijana mdogo sana ila mwenye sauti na ushawishi.....tuliingia mzigoni na akashinda UDIWANI.
Kinyume na hayo ,wengi ni hawa wenzangu wenye MBANGO kwa kukosa UFAHAMU mkubwa wa mambo.
Ona huyu rafiki yangu...FRANCO...elimu yake ni ile ya "kutambuliwa na katiba" [emoji1787]
Ila Mkulungwa ana FEDHA...za kujitofautisha nasi wasomi KAPUKU.
Anaijua mitaa vyema kwani alianza kuhaso sisi tukiwa katika zipu za baba zetu, biashara za haramu zilikuwa zake....halali...kati na kati...leo ana "dinari" maa shaa Allah.
Amewashika wajumbe....na anajua SIASA CHAFU....amewashika CCM kata.....hawapumui kwani majuzi amenieleza jinsi alivyomlipia mmojawao* DENI lake la milioni 6 [emoji1787]
Madambwe ya bodaboda na BAJAJI anatajwa yeye tu....
Vijiwe nongwa vya kahawa kila uchao anavizungukia na kuacha buku 5 kila kijiwe..navijua 6 alivyoviweka mkononi. Vijana wa "PULL TABLE" kila zilipo hizo meza za kucheza kwa kamari.
Misikiti 4 anawasaidia maimamu shida zao ndogondogo. Makanisa madogo ya kilokole mwamba yupooo [emoji1787]
Si misiba ,si Maulid ,si vipaimara ,si visherehe vya "bebi shawa" vya akina Rukia na Mwajuma micharuko....yote haya kisa UDIWANI TU [emoji1787][emoji1787]
Tabia yake :
Kwa nguvu hizo za ushawishi na mkwanja alionao jamaa ANAONGEA SANA...ana MBANGO na mbishi....alichokosa tu ni nidhamu ile inayopatikana tu kwa KUSUGUA SANA MAKALIO katika viti na madesk ya madarasa [emoji1787]
---_---------------------------------
FIKIRI
Mtu afananaye na kaka mkubwa FRANCO ashinde UDIWANI na awe mjumbe wa kikao cha HALMASHAURI uso kwa uso na DC hata kama DC huyo ni mwerevu....ni rahisi sana DC kukasirishwa na maneno makali ya hawa madiwani sampuli ya huyu swahiba yangu....
DC huyo anahitajika awe na "GUTS" ....udume na ujike kweli wa kutawala HISIA ZAKE(emotions) kwani "akitekenywa PUDENDAL NERVE" "atasimamisha" MISHIPA ya shingo na kutoa MACHO na mwishowe KUROPOKA hata yasiyokuwepo....
Kwa kujitetea huku akiwa na GHADHABU yanaweza KUMPONYOKA maneno makali yenye UKAKASI hata YASIYOPATA KUTOKEA kwa UHALISIA wake....
Ndio maana tunazidi kukumbushana "EMOTIONAL INTELLIGENCE". Mwalimu wangu Prof.Masalakulangwa alishawahi kuniambia kuwa "NEVER MAKE DECISION WHILE YOU'RE ANGRY."
Binafsi nasubiri kumuona jamaa yangu atakavyomuangusha DIWANI aliyepo kwani wote wana "elimu" egemeo la katiba *[emoji1787]
Wote wana MBANGO....kazi kwake huyo DC wa wilaya yetu [emoji1787][emoji1787]
Allah awalinde usiku huu ,amen[emoji7]
Alamsiki binnuur [emoji2956]
#Nchi Kwanza