RafikiNdugu: Abdallah Tambaza na Kleist Sykes

RafikiNdugu: Abdallah Tambaza na Kleist Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ABDALLAH TAMBAZA NA KLEIST SYKES
Nafungua gazeti la Raia Mwema nimekuta katika ukurasa maarufu wa Shajara ya Mwana Mzizima makala haya, "Huyu Ndiye Kleist Sykes Meya Aliyebuni Mradi wa Mwendokasi."

Abdallah na Kleist ni marafiki toka udogo wao walipoanza kusoma Al Jamiatul Islamiyya School Mtaa wa Stanley na New Street.

Abdallah na Kleist wote wanatoka katika koo maarufu za Dar es Salaam.

Historia ya Tambaza ni kongwe zaidi inakwenda nyuma zaidi ya miaka 200 na imehifadhiwa na yote inafahamika.

Huwa nacheka wakati mwingine ninapoyasikia majina ya babu zao akina Tambaza walioishi Dar es Salaam kiasi cha miaka 100 na zaidi iliyopita leo yakiwa wamepewa wajukuu na vitukuu.

Abdallah amehifadhi historia yao yote ghibu na kwa maandishi.

Historia ya akina Sykes ni maarufu Dar-es-Salaam ni historia ya miongo 13 iliyojaa siasa za mji khasa Kariakoo baada ya Vita Kuu ya Kwanza.

Kleist kama Abdallah alikuwa akiijua vizuri historia ya babu zake akina Mbuwane na Plantan, mamluki wa Kizulu walioingia German Ostafrika mwishoni mwa miaka ya 1800.

Wakati Abdallah aliijua historia ya wazee wake kwa kupokea kutoka kizazi kimoja hadi cha pili na kwa kuona athari walizoacha babu zake kama mji wa Kisutu na Msikiti wa Mwinyikheri Akida na ardhi kubwa ya Upanga na kwengineko; Kleist yeye historia ya babu zake kaipokea kwa kuisoma ikiwa katika kitabu alichoandika babu yake kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Babu yake Kleist alikuwa mmoja wa waasisi wa African Association mwaka wa 1929.

Baba yake Meya Kleist, Abdulwahid Sykes alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU iliyotokana na African Asociaiton.

Abdallah na Kleist walikuwa rafiki ndugu hadi Kleist alipofariki mwaka wa 2017.
Umri ukisogea na fikra za kukumbuka yaliyopita huja kwa wingi kichwani.

Nasoma makala ya Abdallah anaeleza mchango wa Kleist katika kuleta usafiri wa mwendo kasi wakati alipokuwa Meya wa Dar-es-Salaam.

Babu yake Kleist yaani somo yake, Kleist Sykes Mbuwane alikuwa Mwafrika wa pili kuwa katika baraza la Dar-es-Salaam Municipal Council.

Mwafrika wa kwanza akiwa Sheikh Mwinjuma Mwindadi aliyekuwa Headmaster wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School.

Nayaona masikitiko ya Abdallah kuwa juhudi za Kleist hazijathaminiwa na ukimsoma katikati ya mstari ni kama vile Abdallah anasema iweje mji wao Dar es Salaam, mji waliozaliwa wao na babu zao mathalan utoe majina ya madaraja na mitaa kwa wale wanaowadhania wanastahili lakini wawaweke pembeni wenye mji wao waliofanya makubwa yasiyokuwa na mfano?

Inawezekaje Dossa Aziz asiwe na mtaa Gerezani?

Abdallah na Kleist mimi ni rafiki ndugu zangu ingawa mimi wamenipita miaka miwili mitatu.

Wenzangu hawa ingawa wametangulia kuona jua kabla yangu rika letu ni moja pamoja na ukuzi wetu.

Nitaweka picha za ujana na utu uzima wetu.

Naamini ipo tofauti kubwa na utaona miaka 50 toka tupige picha ya kwanza mwaka wa 1968 imetufanyaje.

Ila hakuna tofauti kwa dada zetu ambao ajabu wao hesabu kwao imesimama.
Wanazidi kupendeza kila uchwao.

Tumeishi pamoja katika mji wa Dar-es-Salaam toka kuzaliwa kwetu kwa hisani na mapenzi makubwa yasiyo na mfano.

Picha ya kwanza mwaka wa 1968 waliosimama kushoto ni Abdallah Tambaza, Bubby, Kleist Sykes, Yusuf Zialor na Mohamed Said.

Waliochuchumaa kulia ni Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kaisi.

Picha ya pili waliosimama kulia ni Mohamed Chande, Mohamed Said, Ami Mpungwe, Lilianne Sykes, Abdallah Tambaza, Erica Kissa, Hassan Ndumbaru, Kleist Sykes, Bubby.

Waiochuchumaa kulia ni Wendo Mwapachu, Hamida Simba na Abdul Mtemvu.

1660767803396.png
1660767831552.png
1660767854166.png
 
Kleist Sykes Mbuwane alikuwa Mwafrika wa pili kuwa katika baraza la Dar-es-Salaam Municipal Council.
Heshima kwako mkuu.

Naomba kufahamu kama huyu kleist ndiye ambaye hivi karibuni mke wake pamoja na kaka yake wanapelekana mahakamani kuhusu kugombania mirathi yake?
 
Heshima kwako mkuu.

Naomba kufahamu kama huyu kleist ndiye ambaye hivi karibuni mke wake pamoja na kaka yake wanapelekana mahakamani kuhusu kugombania mirathi yake?
Bahati,
Kleist ni marehemu toka 2017.
 
Nilifikiri Wendo Mwapachu ni mwanamke,dada yao kina Mwapachu aliyefariki miaka michache iliyopita alikuwa anaitwa nani?
 
Back
Top Bottom