Rage awapa makavu wanasimba

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
NILIIKUTA SIMBA INANUKA MAVI NA MADIRISHA YA MAGUNIA Mwenyekiti
wa Simba Ismail Aden Rage amesema ataiacha Simba katika
hali nzuri tofauti na alivyokabidhiwa wakati uongozi wake unaingia
madarakani. Rage ambaye ametangaza kutokugombea tena uongozi
Simba amesema ameubadilisha uongozi klabuni kwani kulikuwa na
ufisadi na ufujaji wa mali za klabu. "Nilikabidhiwa klabu ikiwa inanuka mavi na Madirisha ya magunia lakini
nitaicha ikiwa kwenye hali nzuri na fedha za kutosha, kuna Mil 100
nitawaambia zinatoka wapi kuna Mil 200 nitawaambia zinatoka wapi."
Alisema Rage Rage pia amesema atamrithisha Mwenyekiti anayekuja
deni la Tsh Mil
480 toka Etol Du Sahel kama Malipo ya mauzo wa Emmanuel Okwi, Katika hali ya Kushangaza Rage alijikuta akisema Kuwa Wanachama
wengi wa Simba ni 'Mbumbumbu', Uongozi wa Rage utafika kikomo Mei
4 2014 pale wanachama wa Simba watakavyochagua viongozi mpya.
 
Mkuu kwa jinsi msomali anavyowatumieni kama atakavyo, nakubali kutokubaliana nawe kuomba radhi.

mkuu siku hizi mapinduzi hayaruhusiwi ndo maana rage anapata kiburi kuna baadhi ya wanachama ndo anawatumia kufanya mambo yake
 
Mbumbumbu mpo? Rage huyu!! Yaani unadiriki kuwaita mashabiki wa timu yako 'mbumbumbu'!! Walikukosea nini mzee mwenzangu? 😇
 
Akili za wanachama woote wa Simba ni robo tu ya mataputapu yaliyomo kichwani mwa Rage.
Aisee! Kutoka 2014, mpaka leo bado akili zao ni mataputapu tu kichwani! Ujio wa Mwamedi ndiyo umewafanya wawe zaidi ya mataputapu!! Kwa sasa wamekuwa na akili za kimpumu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…