Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC Aden Rage, amesema kifo cha Spika wa bunge mstaafu Samwel Sitta ni pigo kwa wapenzi wa klabu ya hiyo kwa kuwa ndiye aliyeshiriki kuitunga katiba ya klabu hiyo
Akizungumza leo Jumatatu Rage amesema huwezi kutaja katiba ya klabu ya Simba bila kutaja jina la Sitta
Rage amesema Sitta wakati wa uhai wake alikuwa mwanachama na mpenzi mkubwa wa klabu ya Simba SC
Amesema kuna kipindi hata jezi za klabu hiyo zilikuwa zinafuliwa nyumbani kwake
Amesema Sitta ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo ambayo mengine ni vigumu kuyataja.
tff inaziogopa simba na yanga,hazikawii kutishia kuhamia ligi ya zenj,pia mechi yao moja inalipa marefa ligi nzima,watendaj wa tff weng ni watu wa timu hzi,ngumu kwenda nao kinyume