Raha ya deni Kulipa: Kwanini watu hukimbilia kwenye mabaraza/mahakama baada ya kuchemka kurejesha benki!

Raha ya deni Kulipa: Kwanini watu hukimbilia kwenye mabaraza/mahakama baada ya kuchemka kurejesha benki!

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Nilikuwa na jambo langu ambalo limeshaisha kwenye haya mabaraza/mahakama kitengo cha ardhi, huwa wateja tunakaa na wanaita kesi ili wahusika wafike sehemu husika.

Kesi zilizojaa ni mtu flani vs NBC, flani vs CRDB, ABC Ltd vs NBC etc. Wakili mmoja akaniambia nyingi zinachelewesha tu mabenki kuchukua mali zao kwasababu wahusika wanakuwa kwenye panic mode ya kupoteza nyumba/mali zao na wanapoteza pesa nyingine kwenye mchakato wa mahakama.

Nionavyo nyingi zinachelewesha migogoro halisi ya ardhi hasa kutokana na ukubwa wa mawakili wanaotumika huwa wanaloby kwa makarani hizi kesi ziwe mapema na za makapuku kukosa nafasi na kupigwa kalenda.

Andiko hili limechagizwa na taarifa ya mwananchi kwa kampuni moja kuangukia pua kwa benki ya equity kwenye rufaa, jopo la majaji watatu waliwasikiliza, waste of resources kwa pande tatu. Mlalamikaji, mlalamikiwa na rasimali za mahakama ambazo wangetumia wengine.
 
Watu wana kimbilia kwenye mabaraza kwakuwa wanajua wajumbe watawasikiliza na kwa kiasi fulani watakuwa upande wao
 
Back
Top Bottom