Raha ya hodi umkute mwenyeji

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
413
Reaction score
90
Hodihodi naingia,JF kuj'achia
moyoni nimenuia,mawazo kuwaletea
Kwanza nawasalimia,nikitokea Songea
Munipokee jamani.
 
Karibu mkuu jisikie vema na kupevuka kimwili na kiakili pindi ukanyagapo tu jf!

Wanamalenga na wahenga wameweka ngome hapa jf wakinena kimang'amuzi ya nera!
 
Hodihodi naingia,JF kuj'achia
moyoni nimenuia,mawazo kuwaletea
Kwanza nawasalimia,nikitokea Songea
Munipokee jamani.

karibu karibu mwana kwetu jisikie uko nyumbani,uhuru wa fikra na upana wa mawazo hapa umefika,karibu karibu mwanakwetu
 
Du umekuja kwa kasi!Nimeipenda hiyo heading yako.Kweli,'raha ya hodi umkute mwenyeji.Karibu habari ya kunyumba?Mahengo?
 
Pastor Achachanda,Kunyumba ena kunyai.Kwani bwana wewe unatokea wapi?Mbona unaongea cha kwetu?
 
Nyoni watoka Songea,majina tumeyazoea,
Kuna Komba Tembo Mbawala na Kima apatikana.
KARIBU SANA KIJANA.
 
kumbuka kuna mwenyeji mwingine waweza umkute lakini asikupe raha. upooooooooooo?
 
Karibu karibu, naona umekuja na mistari km bro wako wa mjengoni, karibu jukwaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…