Raha ya kupanga chumba kimoja

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Unajua bwana kila kitu kina raha na karaha zake. Sasa kupanga na kuishi ndani ya chumba kimoja, kuna raha na karaha zake pia.

Kwa ufupi karaha zake ni kama pale itokeapo ukapata ugeni jinsia tofauti na wewe (siyo mpenzi wako) hapo lazima kichwa iwake

Tukirudi kunako raha za kupanga chumba kimoja, raha ni nyingi, ila raha na duraha iliyo kuu ni pale unapoamka asubuhi, YAANI VITU VYAKO VYOTE UNAVIONA.
 
Ili ndio tatizo la kuamka na njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba imefanikiwa kupata gheto...??

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Mbona kuna walio oa wanaishi chumba kimoja na unaambiwa baba mkwe ni mgonjwa amepata rufaa kwenda Muhimbili kutokea Nanjilinji.

Anakuja yeye na mama mkwe na wanakaa miezi sita. Cha ajabu kabla hawajaondoka wanawauliza mna tatizo gani mbona hakuna dalili ya uzazi.
 
Chumba kimoja? Labda uwe unakula hotel, ila kama maswala muhimu yote unamalizia humo, mende hakosekani na harufu za ajabu ajabu, kuanzia boxer mpaka viporo
Hapana ninapinga hoja. Ukiwa na discipline unaweza. Baada ya kula unaosha vyombo, sufuria ya ugali unaosha juu unabakiza ule ukoko wa chini tu. mboga iliyobaki unaifunika kwenye container.
 
Hapana ninapinga hoja. Ukiwa na discipline unaweza. Baada ya kula unaosha vyomba, sufuria ya ugali unaosha juu unabakiza ule ukoko wa chini tu. mboga iliyobaki unaifunika kwenye container.

Nami napinga hoja, raha ya chumba kimoja kuwe na kitanda , sehemu ya kuifadhia nguo... ndani ya chumba kimoja kupika ni hatari, unaweza choma nyumba ya watu...
 
Nami napinga hoja, raha ya chumba kimoja kuwe na kitanda , sehemu ya kuifadhia nguo... ndani ya chumba kimoja kupika ni hatari, unaweza choma nyumba ya watu...
Tunaishi hivyo wangu, tena tume up grade kila chumba kina jiko la gesi na mtungi wake. Kwenye corridor labda kukaanga samaki tu kwani wana shombo. Shangaa wewe fire extinguishers hatuzijui lakini tunalala na mabomu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…