Raha ya safari za usiku 12Hrs Dar - Shinyanga

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,093
Safari ilikuwa tar 11 Dec kuamkia 12 Dec
Gari, Toyota Allion 1.8L
Wese la laki 2 tu Dar_Shy

Safari ilianza saa 12 jioni, hadi saa 12 alfajiri.

Wadau wengi nilikutana nao barabarani, wakienda maeneo mbali mbali, karagwe, kahama, Mwanza, bukoba, kwa hyo ilikuwa mwendo wa kupeana kampani tu na kusindikizana.

Barabara iko wazi sana, kweupeee hakuna Tochi wala vizingiti..

Speed ni 100 kwa 120.

Tahadhari, ni Umakini mkubwa unahitajika na ukisikia dalili yoyote ya Usingizi park gari ulale. Maroli pia yanapark ovyo barabarani ni muhimu sana kuyaangalia kwa umakini.

Otherwise safari inakuwa tamu sana na unajikuta tu umeshafika sehem kwa muda mfupi sana. Hali ya hewa iko cool barabara imepoa na hakuna Makelele.

Share uzoefu wako hapa pia.
 
Huu ni mwezi wa safari za usiku. Tushauriane kulala mchana baada ya lunch ukiamka ndo uoge na uanze safari. Nakushukuru kama ulitembelea 100-120km/hr. Huu ni mwendokasi mzuri ambao hauwezi kusababisha breaking news lakini kuna vijana wakiona barabara iko wazi wanabutua mpaka 150/180km/hr kama wa magazeti na IT.
 
2009 nilikoswa koswa kutekwa pori la Runzewe usiku kwa ubishi tu,askari uwa wanaweka beria kuzuia gari zisipite usiku kuna majambazi wanatekaji kwenye ilo pori.
Wabishi tulikua jumla gari tatu tukapeana moyo tutasindikizana tukatoa posho,askari wakatutahadharisha kabisa kuna hatari huko usiku sio salama lakini atukusikia.
Safari ikaanza wenzangu wawili wakakamua mafuta mimi na pajero ya urithi nikawa naenda mwendo wa kunyata.

Katikati ya pori kuna konakona umo,kumaliza kona flani hivi nikapiga taa full nikaona watu barabarani na zile gari mbili zimesimama moja ikiwa pembezoni mwa barabara.kumbe tayari wenzangu wamekutana na magogo barabarani,nikasimama kwa mbaali sasa ili nisome kuna nini!!
Majambazi wakajua gari nililosimamisha ni askari wakaanza kurusha risasi huku wakijihami.
Nikaingia porini kidogo nikachekecha gari nikageuza kurudi bila madhara ya risasi kunipata mimi na gari.
Wakati huo kuna dada nimempa lifti siti ya nyuma akanikaba shingoni kwa uwoga tu.

Tangia siku hiyo nikashika adabu kutembea usiku.
 
Safari ilikuwa tar 11 Dec kuamkia 12 Dec
Gari, Toyota Allion 1.8L
Wese la laki 2 tu Dar_Shy

Safari ilianza saa 12 jioni, hadi saa 12 alfajiri.

Wadau wengi nilikutana nao barabarani, wakienda maeneo mbali mbali, karagwe, kahama, Mwanza, bukoba, kwa hyo ilikuwa mwendo wa kupeana kampani tu na kusindikizana.

Barabara iko wazi sana, kweupeee hakuna Tochi wala vizingiti..

Speed ni 100 kwa 120.

Tahadhari, ni Umakini mkubwa unahitajika na ukisikia dalili yoyote ya Usingizi park gari ulale. Maroli pia yanapark ovyo barabarani ni muhimu sana kuyaangalia kwa umakini.

Otherwise safari inakuwa tamu sana na unajikuta tu umeshafika sehem kwa muda mfupi sana. Hali ya hewa iko cool barabara imepoa na hakuna Makelele.

Share uzoefu wako hapa pia.
Wese la laki2 wakati ungepanda bus ungetumia less than 60K
 
2009 nilikoswa koswa kutekwa pori la Runzewe usiku kwa ubishi tu,askari uwa wanaweka beria kuzuia gari zisipite usiku kuna majambazi wanatekaji kwenye ilo pori.
Wabishi tulikua jumla gari tatu tukapeana moyo tutasindikizana tukatoa posho,askari wakatutahadharisha kabisa kuna hatari huko usiku sio salama lakini atukusikia.
Safari ikaanza wenzangu wawili wakakamua mafuta mimi na pajero ya urithi nikawa naenda mwendo wa kunyata.

Katikati ya pori kuna konakona umo,kumaliza kona flani hivi nikapiga taa full nikaona watu barabarani na zile gari mbili zimesimama moja ikiwa pembezoni mwa barabara.kumbe tayari wenzangu wamekutana na magogo barabarani,nikasimama kwa mbaali sasa ili nisome kuna nini!!
Majambazi wakajua gari nililosimamisha ni askari wakaanza kurusha risasi huku wakijihami.
Nikaingia porini kidogo nikachekecha gari nikageuza kurudi bila madhara ya risasi kunipata mimi na gari.
Wakati huo kuna dada nimempa lifti siti ya nyuma akanikaba shingoni kwa uwoga tu.

Tangia siku hiyo nikashika adabu kutembea usiku.
Kwa barabara hzo mkuu ni changamoto hasa kwa sababu zina historia ya matukio kama hayo..kikubwa unapaswa kujua kwanza historia ya eneo unaloenda.

Kwa road ya Dar_mwanza, Dar_Arusha au Tanga, Dar_Mbeya sijawah kusikia habari za kutekana...unless mtu azidishe speed tu
 
2009 nilikoswa koswa kutekwa pori la Runzewe usiku kwa ubishi tu,askari uwa wanaweka beria kuzuia gari zisipite usiku kuna majambazi wanatekaji kwenye ilo pori.
Wabishi tulikua jumla gari tatu tukapeana moyo tutasindikizana tukatoa posho,askari wakatutahadharisha kabisa kuna hatari huko usiku sio salama lakini atukusikia.
Safari ikaanza wenzangu wawili wakakamua mafuta mimi na pajero ya urithi nikawa naenda mwendo wa kunyata.

Katikati ya pori kuna konakona umo,kumaliza kona flani hivi nikapiga taa full nikaona watu barabarani na zile gari mbili zimesimama moja ikiwa pembezoni mwa barabara.kumbe tayari wenzangu wamekutana na magogo barabarani,nikasimama kwa mbaali sasa ili nisome kuna nini!!
Majambazi wakajua gari nililosimamisha ni askari wakaanza kurusha risasi huku wakijihami.
Nikaingia porini kidogo nikachekecha gari nikageuza kurudi bila madhara ya risasi kunipata mimi na gari.
Wakati huo kuna dada nimempa lifti siti ya nyuma akanikaba shingoni kwa uwoga tu.

Tangia siku hiyo nikashika adabu kutembea usiku.
Mkuu miaka mingi sana imepita. Kwa Sasa tunatembea vizuri tu
 
Nilitembea masaa matatu tu,toka Singida Mjini hadi taa za pale Shinyanga hapo karibu na posta nafikiri.
IMG_20211118_123056_3.jpg
 
2009 nilikoswa koswa kutekwa pori la Runzewe usiku kwa ubishi tu,askari uwa wanaweka beria kuzuia gari zisipite usiku kuna majambazi wanatekaji kwenye ilo pori.
Wabishi tulikua jumla gari tatu tukapeana moyo tutasindikizana tukatoa posho,askari wakatutahadharisha kabisa kuna hatari huko usiku sio salama lakini atukusikia.
Safari ikaanza wenzangu wawili wakakamua mafuta mimi na pajero ya urithi nikawa naenda mwendo wa kunyata.

Katikati ya pori kuna konakona umo,kumaliza kona flani hivi nikapiga taa full nikaona watu barabarani na zile gari mbili zimesimama moja ikiwa pembezoni mwa barabara.kumbe tayari wenzangu wamekutana na magogo barabarani,nikasimama kwa mbaali sasa ili nisome kuna nini!!
Majambazi wakajua gari nililosimamisha ni askari wakaanza kurusha risasi huku wakijihami.
Nikaingia porini kidogo nikachekecha gari nikageuza kurudi bila madhara ya risasi kunipata mimi na gari.
Wakati huo kuna dada nimempa lifti siti ya nyuma akanikaba shingoni kwa uwoga tu.

Tangia siku hiyo nikashika adabu kutembea usiku.
Interesting
Vipi hao jamaa mlio ongozana nao, ulipata mrejesho wowote nini kiliwasibu?
 
Nina experience mbaya na safari za usiku, 2016 tulitekwa na wale wa kuweka magogo barabarani kati kati ya Same na Mwanga.
Safari ilikua Arusha to Dar, tulitoka Arusha sa 6 kasoro usiku, waliharibu sana gari kwa kuvunja vioo ila tunashukuru hawakutudhuru hata zaidi ya kutuchukulia vitu vyetu.

Ilinichukua muda kidogo kupona ile hofu ya lile tukio na nimekua muoga hadi leo wa kusafiri usiku.

Hahaa nakumbuka baada ya lile tukio hata sherehe za usiku nikastop kuhudhuria almost a year maana likiingia giza kama sijarud home hofu inatanda😅
 
Back
Top Bottom