Raheem sterling: Kijana aliyekuwa super sub sasa anafukuza mwizi kimya kimya!

Angalia gharama zao za kusajiliwa unaweza kuelewa uwezo wao uwanjani kama ulikua huwafahamu kabla ya kusajiliwa na m.city
Nafahamu vizuri sana...
Pia katika usajili uliowahi kupondwa ni usajili wa John Stones,watu walisema hastahili kununuliwa kwa pesa ambayo Man City wameitoa...
Kwanini watu waliponda..?
Kwasababu John Stones alikua ni beki wa kawaida sana,pia msimu uliopita wapinzani wa Pep walimsema sana vibaya Stones kwa makosa kadhaa aliyokua akiyafanya uwanjani..!

Pia usisahau kuwa nafasi ya asili ya Fabian Delph uwanjani ni kiungo,ila Pep Guardiola ameanza kumtumia kama LB,tangu ameanza kucheza nafasi hiyo amekuwa bora zaidi ya alivyokuwa awali..!

Ndugu ubishi haukusaidii chochote...
Stones unayemuona sasa ametengenezwa na Pep...
Ni tofauti sana na yule John Stones wa Everton..!
Fabian Delph unayemuona sasa Man City si yule wa Aston Villa..!
 
Unaweza kuwa sawa sehemu flani ila pia hauko sawa sehemu flani

Stones ni beki mzuri ndomana city wakatoa mil 50 angekuwa sio mzuri asingecost kiwango hicho cha hela, na sio city tu ndo walikuwa wanamtaka kumbuka ata Chelsea na man u walikuwa wanahitaji huduma yake ila stone akachagua city

issue ya pep kumfanya awe bora sio kweli bali amejua kumtumia vizuri ila alikuwa teyari bora na alikuwa anastahili kununuliwa bei kubwa kulingana na soko lilivo saizi na bei zake za ajabu ajabu, kwa upande wa fabian hapo sina tatizo kusema pep amefanya kitu kikubwa kumbadili position na jamaa kufit
 
Mkuu we ni shabiki wa liver kweli? Yaani hujui hata raheem aliondokaje unasema tunajuta kumuuza? Liver mchezaji ambae walijuta kumuuza ni Robbie Fowler
Walikuwa wanamwita god of goals.
 
liverpoll tunajuta kumuuza huyu kijana-yani ile TRIPLE S yetu ya suarez,sterling na sturridge ni sturridge pekee ndio afanyi vizuri
Alilazimisha kuondoka kwenda kutafuta changamoto pamoja mataji,wakati yeye na Henderson suala la mikataba yao lilikuwa mezani kwa Ian Ayre ila hakuonyesha subra na alihitaji mshahara mkubwa
 
Liver damu na cjawah kummiss sterling hats sekunde na haitokaa itokee.akafie mbeleee hukoo
 
Najaribu kumkumbuka Raheem wa Liverpool…Raheem wa Brendan Rogers..Aliye mchachafya Kolo Toure pale Anfield katika sare ya 2-2..Sterling alimkimbiza mkonge Kolo Koure na kumchachafya kidogo..Hiyo ilikuwa msimu wa 2012-2013..

Msimu uliofuata Raheem aliendelea kujitengenezea jina chini ya Rogers..Ni msimu ambao Raheem alitengeneza combination nzuri sana na Coutinho na Suarez..Nakumbuka alichaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji kijana wa Epl 2013-2014..Alikuwa miongoni mwa wachezaji sita walio wania tuzo hiyo lakini mwishowe Eden hazard akanyakua tuzo hiyo..Suarez alipata tuzo ya mchezaji bora wa EPL(PFA player of the year)…Lakini Raheem alishinda tuzo ya mchezaji bora kijana wa msimu ndani ya Liverpool

Baada ya msimu wa 2014-2015 aliamua kuondoka Liverpool na kujiunga na man city..Hii ni baada ya kusumbuana sana na Liverpool juu ya mkataba mpya..

Chini ya Pellegrini Raheem msimu wa kwanza hakuingia moja kwa moja kwenye timu..Alipata injury ambayo ilimpelekea kukaa nje kwa wiki nane hivyo kumfanya kupotaza nafasi yake katika kikosi…Haukua msimu mzuri sana kwake..Pia hata msimu uliopita chini ya Pep bado Raheem hakuwa bora sana..Yawezekana ni kutokana na timu ya Man city kwa ujumla kutokuwa imara sana msimu uliopita ikizingatiwa kuwa ndio ulikuwa msimu wa kwanza kwa kocha mpya ambaye alikuja na falsafa mpya ya kuuchezea mpira na kushambulia muda mwingi wa mchezo

Msimu huu umekuwa mzuri sana kwa huyu kijana..Amefunga magoli 14 mpaka sasa Epl..Ana enjoy sana huu mfumo wa Pep wa kushambulia kwa kasi sana..Jamaa ni aina ya wale viomoro wanaopendwa na Pep..Speed yake ni silaha kubwa inayo wafanya Silva na De bruyne kupitisha mpira katika nafasi na yeye kumalizia..

Naamini huu ndio msimu ambao Raheem amekuwa katika kiwango cha juu Zaidi katika Maisha yake ya soka..
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Nilimuona Delph akiwa Aston Villa pia nilimuona Stones akiwa Everton...
Wote walikua ni average players...
Bila kusahau Fabian Delph hakuwa anacheza nafasi ya LB akiwa Aston Villa..!
Una swali lingine..!?
Jipe moyo city wanachukua average player toka lini??
 
Jamaa kamla mke wa Gabriel mpk demu kajifungua kitu black
 
liverpoll tunajuta kumuuza huyu kijana-yani ile TRIPLE S yetu ya suarez,sterling na sturridge ni sturridge pekee ndio afanyi vizuri
Liverpool imekuwa sehemu ya wachezaji kuonekana..badala ya hao wachezaji iipe kikombe Liverpool...

Naona kwa mbali hata mwarabu hana maisha marefu Lvrpool
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…