Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Kuna ubishi wa chini chini kati ya hawa mabinti wawili machachari ambao ni zao la Jahazi Modern taarab chini ya aliyekuwa mkurugenzi wao mfalme Mzee Yusuph ,je yupi ni mkali zaidi kuliko mwenzake?.
Hakuna ubishi, Rahma Machupa ukipenda muite Messi na Fatma Mahmoud ukipenda muite Fatma Nyoro wote ni wakali kwenye kushambulia jukwaa na kwenye uimbaji.
Messi aliwahi kutamba na wimbo wa Nipe Stara alipokuwa na bendi ya Jahazi Modern Taarab, kwa sasa anatamba na wimbo wa Wanabweka sana lakini hawang'ati kwenye bendi mpya ya Nakshi Nakshi Modern Taarabu wakiwa sambamba na Mwasiti Mbwana, Mohamedi Mtu pori na Father Mauji.
Fatma Nyoro aliwahi kutamba na nyimbo kama vile Marupe rupe,Aso kasoro ni Mungu, kwa sasa anatamba vyema na wimbo wa Siwaguni Siwakohoi chini ya bendi ya Yah TMK.