RAI - Nguvu ya Hoja?

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Hii imetoka kwenye RAI la tarehe 18-24 Septemba 2008, toleo namba 782.

I remain speechless!

 

Attachments

  • RAI0908.png
    40.2 KB · Views: 4,535
Huu ni mpambano wa vyama kupitia vyombo vya habari.Sikutegemea kama Rai wangeweza kujiweka wazi kiasi hiki kuwa linapigia upatu ccm na serikali yake kwani usipokuwa makini unaweza kufikiri unasoma Uhuru. Ya kwetu majicho
 
Invisible,
Thanks for this. Kwa mantiki yao Slaa kuibua suala la ufisadi wa EPA ni kuendeleza siasa za kuchafuliana. Very interesting.
 
Nimesoma RAI tangu kifo cha WANGWE hawa jamaa kwenye frontpage au maoni ya mhariri lazima waandike habari za kuibomoa CHADEMA ngoja nikusanye nakala ya heading nitaziandika muone wenyewe
 
sio kosa lao rai.tatizo wanashinikizwa na boc wao RA.Watanzania tufike mahala tujiulize je mafisadi wanafurahia juhudi za CHADEMA kupambana na ufisadi?kama hawafurahii basi ni dhahiri kabisa watatumia njia yeyote wawezayo kuhakikisha wanaua mapambano yanayoendelea dhidi ya ufisadi.
 
JF inatumika kumchafua Kikwete?!?!?! Oh! Nadhani that is one of the reasons why inv. amekuwa speechless
 
Nimeiona ile ya mtandao wa wanasiasa uchwara na wana habari mamluki ndani ya JF nikamfikiria rafiki yangu Mwkjj. Kwi!kwi!kwi!
 
Narejea kulekule,

Mhariri kama mhariri amesomea taaluma yake. Siwezi kamwe kumvisha lawama mmiliki wa chombo cha habari kwa kumlazimisha mhariri kuandika madude na akakubali kwa kuendekeza njaa zake.

Niliyasema haya wakati watu walipokuwa wakimtwisha Mengi upuuzi wa vyombo flani vya IPP nikisema wa kuwakemea ni waandishi wetu ambao wanakuwa short cited na maslahi ya nchi.

Hakuna wa kuua mapambano dhidi ya udhalimu na wizi wa aina yoyote. Nyakati za sasa si za enzi zile. Ni ngumu kwa wakati huu.

Ninachoweza kusema zaidi ni kuwa Rostam hastahili lawama kwa njaa za waandishi wake wasiozingatia maadili!

Mwisho, JF haina udugu na CHADEMA kama ninavyoona wengine wanakuwa na hoja za "Ukiigusa CHADEMA basi JF inageuka mbogo"... Labda niulize: Who is JF? Atakayejua maana ya JF basi ataelewa yeye ni nani ndani ya JF na kwanini ajiite CHADEMA au CCM.

Mapenzi ya wadau mbalimbali ndani ya JF si msimamo wa JF hata chembe. Binafsi (Invisible) siamini kama nikiwa na mtizamo tofauti na Dr. Slaa au Makamba nitachukuliwa adui au mpinzani wao.

We Dare To Talk Openly, wanaoutumia uhuru vema basi wanaweza kuelewa what we mean!
 
Tanzania kweli tumefika Hapa...??
Hahaha Yebo Yebo,

YES, ndipo vyombo vyetu vya habari vinakoelekea. Kwa anaye-read between the lines atapata undani na dhamira ya mwandishi. CHADEMA wenyewe waki-misread basi wanaweza kujichanganya!

Target ya Balile imenichekesha sana... Uzuri naye ni member wa JF!
 
JF inatumika kumchafua Kikwete?!?!?! Oh! Nadhani that is one of the reasons why inv. amekuwa speechless
Na mtu wa kwanza kunifahamisha kuwa kuna article ndani ya RAI imeandikwa ndivyo sivyo (kwa njia ya barua pepe) ni insider na member wa JF ambaye yumo humu kila kukicha, anaelewa the issue behind these stories!

Kila anayepinga chochote au anayekosoa basi anaipaka matope serikali.

Serikali yetu inatambua sana kuwa kuna waandishi wa namna ya Balile, inatambua kuwa ukishangiliwa sana utambue kuna wakati utazomewa! Mangapi mazuri na pongezi ngapi zimeandikwa humuhumu na kwanini Balile asiziongelee walau?

Kuna wanasiasa uchwara? Hili ni tusi kwa wengi sana!
 
Last edited by a moderator:
Huu ni mpambano wa vyama kupitia vyombo vya habari.Sikutegemea kama Rai wangeweza kujiweka wazi kiasi hiki kuwa linapigia upatu ccm na serikali yake kwani usipokuwa makini unaweza kufikiri unasoma Uhuru. Ya kwetu majicho

Tehe tehe, eti mpambano wa vyama, acha hizo na kutuzuga. Huu ni Mpambano wa MAFISADI (ROSTAM NA LOWASSA) NA WAZALENDO
 
Mhariri Mkuu wa Rai ni BALILE,na ndiye aliyeandika tahariri hiyo.Alikuwa member wa JF,nadhani hadi sasa,wakati anasoma hapa Hull.Sasa wandugu,zama za kulalamika bila vitendo zimepitwa na wakati.Huyu jamaa anatumia gazeti lake kuikashifu JF na kuibebesha tuhuma nzito ambazo kama tutazikalia kimya zinaweza kuonekana kuwa ni facts.

Mawazo jamani,tumfanye nini huyu Balile?
 
Nimesoma RAI tangu kifo cha WANGWE hawa jamaa kwenye frontpage au maoni ya mhariri lazima waandike habari za kuibomoa CHADEMA ngoja nikusanye nakala ya heading nitaziandika muone wenyewe

Kipekee tunawashukuru RAI kwa kujianika waziwazi na kila mwenye akili timamu anaona kuwa RAI ni mdomo wa pili wa CCM na serkali yake.

Tangu ROSTAM alinunue gazeti hilo na mengineyo ktk kampuni hiyo vyombo hivyo vimekuwa vikijitahidi kwa hali na mali kuandika vibaya kuhusu CHADEMA.Haiingii akilini kuwa gazeti linaandika kukashifu au kuzima ukweli kuhusu tuhuma za ufisadi.

Kuita mtandao wa jambo forum ni waandishi uchwara haimtishi yeyote.Swali ni kujiuliza yupi mwenye afadhali kati ya mwandishi anayetumiwa ili hali anajua anatumiwa kwa matakwa ya MAFISADI na yule anayejitambua na kutafuta uhuru kusema yaliyo ya kweli?

Kwa wanaosoma Tanzania Daima na magazeti mengine yasiyoyumbishwa na vijisenti vya watu tunaelewa kuwa tofauti iliyopo kati ya RAI,MTANZANIA na magazeti hayo mengine ni kubwa sana.RAI LINATUMIWA NA LIMEKUBALI KUWA MDOMO WA MAFISADI NA WANASIASA WASIOPENDA KUANDAMWA KWA MAKOSA DHAHIRI.
 

BWA HA HA HA HA NAVINJARI JIKONI NA CHUMBANI MWAKE SI KITAMBO!!!!!!!!!!!!!!!!!! chungu kuu halikosi ukoko
 

Tufungue kesi mahakamani ili haki itendeke... au kama kufanya hivyo tunaona tunachelewa tuchukue Dr Slaa's Mwembeyanga style!
 
Mawazo jamani,tumfanye nini huyu Balile?

Ukijiingiza katika mabishano na kichaa, watu wanaweza wasijue ni nani kichaa kati yenu. N ainapotokea kichaa akapewa rungu, mabishano hapo yana hatari zaidi
 
Tufungue kesi mahakamani ili haki itendeke... au kama kufanya hivyo tunaona tunachelewa tuchukue Dr Slaa's Mwembeyanga style!

chini kwa chini juu kwa juu mimi sihitaji mahakama, yangu ni mahakama dunia. mkuki kwa nguruwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…