Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
Wasalaam, Ukienda duniani kokote katiba ya nchi ndio sheria mama( mother law). Kwanini ni sheria mama, je watanzania tunajua maana ya katiba?
Ukisoma historia mungu alimuumba Adam, kisha akamnyia mke Hawa, akawapa sheria na miongozo ya namna ya kuishi.; kukawepo hukumu na haki.(kaini alimuua ndugu yake abili: Biblia). Baadae Mungu Baba alimwamuru nabii MUSA kuziandika sheria kwenye mbao za mawe(AMRI KUMI). Hii inajibu swali kwanini katiba ni sheria mama; yani ni mwongozo jamii Fulani iliojiwekea km sheria.
Tanzania mpaka Leo tunatumia katiba ya mwaka 1977 km ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara( viraka). Katiba hii ina misingi ya chama kimoja ambapo mwaka 1992 I litanyiwa marekesho kuongeza kifungu cha kutuhusu uwepo wa vyama vingi vya siasa. Katiba hii iliruhusu uwepo wa time huru ya uchaguzi; hapa tatizo sio tume huru ya uchaguzi, tatizo ni namna tume huru inavyopatikana. Tume hii yote kuanzia MWENYEKITI wake hadi wasimamizi wa uchaguzi wanachaguliwa na na MTU mmoja ambae pia ni MWENYEKITI wa ccm; (hapa ndo kuna ukakasi)
Swali langu hapa ni kwanini ccm inahofu ya kuandika katiba mpya? Je wameona ndo itakua mwisho wa ccm? Hapa Watanzania tukumbuke mchakato wa KATIBA MPYA YA MZEE WARIOBA umegharimu mabilion ya shilingi ambazo ni kodi za watanzania; kisha umetupya kwenye box LA taka. Kwanini ccm kama wanania njema na Taifa hili ( Mh Mbatia huita MAMA TANZANIA) kwanini wasimalizie mchakato wa katiba hata ile ya Mzee Sitta ambayo waliipitisha wenyewe ili kuwe na tume Huru ya uchaguzi, mahakama huru na bunge huru?.