Breakfast:
Maziwa au flavoured yoghurt na muesli/oats unaweza kuweka na matunda kama ndizi,embe au strawberries au matunda mengineyo.Unaweza kutengeneza flavoured yoghurt mwenyewe kwa kupiga mtindi na matunda/tunda upendayo na sukari au asali kidogo.
View attachment 155270View attachment 155271
1 glass orange juice(fresh)
AU
- French toast,mkate ulochovya kwenye mchanganyiko wa mayai na kukaangwa
- sausage mbili zilizokaangwa,
- kipande cha nanasi na tikiti maji
- glasi ya maziwa
Lunch
Spagetti/macarroni na mchuzi wa nyama ya kusaga.
Mchuzi wa nyama ya kusaga:
- Nyama ya kusaga 1/2 kilo,weka kitunguu saumu na tangawizi kijiko kimoja cha chai na uichanganye vizuri,ongezea chumvi na pilipili manga.
- Kaanga kitunguu kimoja kilichokatwakatwa kwenye mafuta kiasi,kikibadilika rangi na kuwa hudhurungi weka nyama ya kusaga na uikaange nayo mpaka iive.
- Weka mbogamboga kama Karorti na viazi zilizokatwa vipande(boxes) ,njegere zilizomenywa,kaanga kwa dakika tano viive,
- Weka nyanya tano zilizomenywa na katwakatwa au zisage kwenye blenda na maji kidogo.Funika na wacha uchemke,
- Ukikaribia kuiva weka pilipili mboga na majani ya korriander,adjust chumvi
View attachment 155273
Unaweza kusev huo mchuzi wa nyama ya kusaga pia na mashed potatoes au wali au upike mchuzi wa nyama ya kawaida
MASHED POTATOES
- chukua viazi kadhaa kama vinne vinne vimenye kisha vichemshe na chumvi.
- Vikiiva vimwage maji kisha viponde mpaka vilainike.
- Weka maziwa na siagi ili kuongezea ladha huo mchanganyiko wako.
View attachment 155274
AU
Lasagne,mchuzi kama wa nyama ya kusaga lakini unahitaji lasagne plates pamoja na cheese.
View attachment 155272
Serve dinner pamoja na fresh salad na maji kama kinywajia
Supper/mida ya saa kumi
Sahani ya matunda tofauti yalokatwa vipandepande(
FRUIT SALAD).Au tengeneza fruit smoothie ya matunda mchanganyiko kama mananas,maembe,machenza,n.k piga na juice ya apple au nyingeneyo.
View attachment 155276View attachment 155277
Dinner
Pancakes with strawberries and cream and honey
Pancakes
Mayai 4
Unga wa ngano 60g
1/2 cha chumvi
Kijiko kimoja cha chai cha vanilla sugar
Maziwa 1/2 dl
Vijiko vitatu vya siagi iloyeyushwa
300g cottage cheese
Vikishaiva weka cream,strawberry na asali juu ya pancake tayari kwa kuliwa
View attachment 155275
Serve na maziwa ya vuguvugu au passion fruit juice.
AU
Viazi vya kuchoma na kuku/vipapatio vya kuku
Osha viazi /ukipenda menya na ukate boats mapande mapana tu vichemshe kama dakika 5 na chumvi,kisha nyunyizia mafuta na uvibake kwenye oven mpaka viive na vibadilike rangi.
Weka viungo uvipendavyo kwenye kuku au vipapatio na uvichome kwenye oven pia
View attachment 155280View attachment 155281
Serve pamoja na salat ya matango,nyanya na carrot!