Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuwasili Tanzania kesho Februari 7, 2026 kufanya ziara ya siku moja

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuwasili Tanzania kesho Februari 7, 2026 kufanya ziara ya siku moja

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anatarajiwa kuwasili Tanzania Februari 7, 2026 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan ambapo mazungumzo yao yatajikita kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kujadili masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

1770365870036.png

Museveni.jpg
 
kama dpworld wampewa bandari ya tanga pia ina maana mwarabu ndiye atakayekusanya mapato yatokanayo na usafirishaji wa hayo mafuta na siyo serikali ...
 
Nilitaka kuhoji swali kuhusu mwenyeji wake iwapo atakuwa amerudi kufikia hiyo kesho, bahati nzuri limejibiwa kupitia hiyo taarifa ya Kurugenzi ya habari ya Ikulu.

Sisi kama JF, tunaye mwakilishi wetu Pascal Mayalla najua atauliza maswali kwa niaba yetu hususani hili la kufungia blogs na mitandao ya kijamii inayo-critisize Serikali kama walivyoifungia Jamii forum kwa muda usiojulikana
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anatarajiwa kuwasili Tanzania Februari 7, 2026 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan ambapo mazungumzo yao yatajikita kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kujadili masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

Anakuja kuchota " maarifa" ya KUUA HALAIKI
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hapo kesho Rais Wa Uganda Atatua Nchini katika Ziara ya Kikazi ya Siku Moja. Ambapo Atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wetu juu ya masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Sisi sote pamoja na ushirikiano wetu wa kihistoria.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Screenshot_20260206-202156_1.jpg
 
SWALI LA KWANZA.KWNN UMETOA ASKARI WAKO KUUA WATANZANIA OCTABA 29
 
Back
Top Bottom