Rai yangu Kwa Mwenyekiti KIFICHO:..Kuahirisha BUNGE:- DHAMBI MBAYA sana..

Rai yangu Kwa Mwenyekiti KIFICHO:..Kuahirisha BUNGE:- DHAMBI MBAYA sana..

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
910
Mwenyekiti

Tokea umeanza KaZi yako ya kuliongoza Bunge hili la KATIBA Binafsi nimeshuhudia Hekima yako kubwa sana unaposhika usukani huu. Na hakika Kwa Kweli umetukumbusha Enzi Za Spika Adam Sapi Mkwawa. Kingine Bunge Lako hili pamoja Na Kamati yako ya Muda ya kuzishabia kanuni Za Bunge wameonyesha uzalendo Na Usikivu kutokana Na maoni mbalimbali ya wadau tuliopo nje ya Bunge. Hii inatutia Moyo kuendelea kutoa rai, ushauri HATA maonyo pale tunapohisi pana JAMBO haliendi Vema ..

Mweshimiwa Mwenyekiti, Mbali Na Sifa nilizokumiminia ila pana suala moja Baya sana lililo Na linalo kiyumbisha vibaya sana kiti chako, nadhani Ni Muda muafaka Sasa wa kulipatia mwarobaini wake wa kudumu. suala hili la KUAHIRISHA-AHIRISHA Bunge Mara Kwa Mara Ni BAYA NA DHAMBI KUBWA KABISA. Mbali Na gharama za kibunge zinazo potea lakini pia hamko peke yenu Mtu 629 Kwenye kichumba hicho bali likumbukeni Kundi kubwa la Watanzania Ndani Na nje ya Nchi Hii wanaofuatilia mtanange huu hatua Kwa hatua. Wapo watanzania wengi Ndani ya nchi wameweka tv maofisini, madukani HATA Kwenye magari yao. Wapo Watanzania nje ya nchi wametumia Fedha zao kuwekeza mitambo mizuri ya Kufanya "U-streaming " walione Bunge live kupitia TBC1 . Uahirishaji wa Bunge haukubaliki Na ukiendelea Basi hautavumilika. Tunajiuliza Kama Leo Hii Kwenye Dibaji tu Bunge linaahirishwa zaidi ya Mara Tano Je wakati wa kuianza KaZi si kuahirisha kutapililiza zaidi!!

Mwenyekiti katika ahirisha yote ha Bunge hapana Sababu HATA Moja ya Msingi. Lazima uelewe hili Mwenyekiti Kwamba Hapo panatungwa KATIBA ya Nchi, sio kitu LELEMAMA. Ni wajibu nguli. Bunge Lako limemeza wasomi Na mangumbaro, wanaojifanya wanajua Na wapole ila werevu, wapigadebe Na watu makini, wavumao na wasiovuma ila wamo. Usitarajie Watu wote 629 wana Akili moja. Wengine hapo Mbali Na Shughuli Za Kibunge ila Binafsi wana Mastress mengi tu, labda wameachwa Na wake zao/waume. Wana madeni HATA kiposho hicho hakija saidia kupunguza mizigo ya madeni, wengine wamekimbilia bungeni Baada ya kukimbia majibu ya Daktari, wengine literary Ni wagonjwa Na wadhaifu sana Na hawana ham ya chochote kinachoendekea vyovyote Kwao Sawa tu.

Lakini kuna wengine Tokea wamezaliwa Hadi makamu ya Utu Uzima Ni wabishi, much-know sana, Tabia Za Ajabu Ajabu . Mbaya zaidi Ni pale misimamo waliyokuja nayo wajumbe kutoka Kwenye VYAMA vyao au wake/waume zao inapochanganyika Kwenye Bunge Lako. Mwenyekiti hili Ndo Bunge Ulilo nalo, sio malaika hao Ni watu, usilazimishe wawe malaika waache hivyo hivyo Kama binaadam wenye utashi Na Mawazo Tofauti.

Mwenyekiti acha kikao kiendelee, acha watu watoe maoni wanavyotaka, acha moto uwake, acha Ngumi zirushwe Kwa wale wataojisikia wala Mtu asiamulie Na wala Askari wasiingie bungeni. Mbunge atayetolewa mchuzi anapelekwa hospitalini Na Bunge linaendelea. Na Muda wowote unaopotea AMA Kwa ndondi au vurugu yoyote au uwakilishaji Hoja ambao hauko Kwenye hadidu Za siku unafidiwa baadae. Kama mpira wa Miguu vile. Potelea Mbali HATA Bunge likienda Hadi saa Tisa Usiku ..Lengo Mzigo wa Siku Ufike.

Mweshimiwa Mwenyejiti kuna baadhi ya wabunge wana Tabia mbaya tu, wako ivyo hawakuanza Jana Na wala huwezi kuwabadili Leo. Ila wapo wenzao wa Tabia mbaya vilevile Kama wanajisikia kuchapana makonde kwanini kuwazuia waacheni wachapane mshindi anaketi kuendelea Na Bunge Na alopigwa anawahishwa medical akipata nafuu anarudi bungeni kutafuta kipigo kingine. Tunatunga kitu kikubwa kitachodumu miaka Mia ijayo, matukio laini Na magumu lazima tuyashuhudie.

Panga Hadidu Za Siku Na simamia kuhakikisha marejesho ya 100% Kwa siku . Ni wiki la Tatu Sasa hakieleweki kitu Mwenyekiti.
 
Yote uliyoandika ni kweli. Hili sio Bunge la Katiba bali ni vituko.
 
Yote uliyoandika ni kweli. Hili sio Bunge la Katiba bali ni vituko. Ushauri mzuri ni kuwa walitakiwa wote kupelekwa milembe na kufanyia mkutano huko wakiwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa akili.

Hawa watu wanahitaji msaada mkubwa sana wa tiba. Tuwasaidieni kwa hilo jamani.

ni kama comedy Fulani hivi!!!!
 
Back
Top Bottom