Ernesto Che
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,114
- 293
Wadau.
NIMEKAA nikitafakari utendaji wa idara yetu ya Usalama wa Taifa. Hii ni taasisi muhimu sana kwa usalama wa nchi na wananchi wake, nchi zote idara hii ina heshima kubwa ndani ya jamii.
Kwa miaka mingi tangu uhuru wan chi yetu imekuwa na taasisi ya Usalama wa Taifa iliyo imara. Japokuwa mengi mabaya yalifanywa kipindi hicho na idara hii, lakini muktadha wangu naujenga kuhusu Hadhi na Heshima ya idara hii nyeti.
Hivi karibuni Usalama wa Taifa (idara) imeingia katika misukosuko kadhaa na wananchi wakiwemo wanasiasa. Mifano michache ni:
Hoja yangu
Idara hii ni muhimu sana, tena yenye heshima na hadhi kwa jamii, ifanye kazi ya kuhakikisha nchi iko salama ili matukio yanayoonyesha udaifu wa mfumo wa kuilinda nchi yetu yasitokee. Mfano Waethiopia wanavuka mpaka na kufia Dodoma katikati ya nchi, je wangekuwa maadui nchi ingesalimika? Je meli zetu zinapata ajali kila mara hakuna hujuma? Madini yanaibiwa na wahujumu uchumi wao wanafanya nini?
Rai yangu kwa usalama wa taifa ni kutoa kipaumbele maslahi ya Taifa sio kulenga kuwaua viongozi wa upinzani (kama kweli madai ya Dr Slaa)

- Mwaka 2010 baada ya uchaguzi, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema Dr Slaa alitoa shutuma za waziwazi kwa idara ya Usalama wa Taifa kuhusu kuhusika na wizi wa kura na kuingilia mchakato mzima wa uchaguzi ili kuipendelea CCM. Siku chache baadae Afisa mmoja wa Usalama wa Taifa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari AKIKANUSHA.
- Tukio la Dr ulimboka limeiingiza idara ya Usalama wa Taifa tena ikiwataja moja kwa moja maafisa wake kutoka Ikulu, hakuna maelezo ya kutoka toka Ikulu kwenye hili
- Mbunge wa chadema (aliyevuliwa) Mh. Godbless Lema alitoa tuhuma kwamba hukumu ya kumvua ubunge ilitokana na maagizo ya Ikulu (Usalama wa Taifa ndio wahusika)
- Dr Slaa/ Mnyika wametoa shutuma za waziwazi wakiwataja maafisa wa Usalama wa Taifa kutaka kuwadhuru kwa staili mbalimbali