Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Inadaiwa kuwa mchungaji wao aliwaambia kwamba wangekutana na Yesu Kristo baada ya kufunga kwa siku 40.
Operesheni ya pamoja ya polisi sasa inaongoza msako wa kiongozi wa kikundi hicho, Simon Opolot.
Inasemekana kuwa wanachama 80 wa Kanisa la Wanafunzi wa Kristo waliacha mali zao zote mapema mwaka huu na kisha kusafiri kutoka eneo la vijijini mashariki mwa Uganda kwenda Ethiopia Kusini, umbali wa takriban kilomita 500 (maili 320).
"Mchungaji huyo anadaiwa alidanganya kwa kuwaambia kuwa wanapaswa kufunga kwa siku 40 ili waweze kukutana na Yesu siku ya 41," Simon Mundeyi, msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Uganda alinukuliwa na gazeti la Daily Monitor akisema.
"Hali ilikuwa kwamba ili kukutana na Yesu, walihitaji kuwa Ethiopia, na kwa mujibu wake, mwisho wa dunia ungefika
Lakini mara tu mamlaka za Ethiopia zilipojua kuhusu kuwasili kwao mwezi Machi, walichukuliwa na kuhudumiwa hadi kurudishwa nyumbani, ripoti ya shirika la habari la AFP inasema.
Bwana Mundeyi alinukuliwa na Daily Monitor akisema kuwa wanachama wa kikundi hicho, wengi wao ni walimu na watumishi wa umma na walikuwa tayari dhaifu sana baada ya safari ndefu bila chakula chochote
Chanzo: Daily Monitor