"Raia Mwema" haiko Mitaani?

"Raia Mwema" haiko Mitaani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Baada ya kutoka na habari motomoto wiki iliyopita (Safari za JK Utata) na nyingine nzito, nimeamka nikikutana na email kibao za watu wakiuliza "Raia Mwema iko wapi". Je kumekuwa na upungufu wa uchapishaji, halikutoka kama imetarajiwa au litatoka late?

Mchuuzi mmoja amedai waliambiwa watapata mchana na sasa ni jioni hawajaliona, Have you seen Raia Mwema today?
 
Halijatoka leo!

kwa mujibu wa wauza magazeti wanasema leo wameambiwa kuwa gazeti la Raia Mwema halijachapishwa kabisa, kifupi halipo mtaani.

kuna tatizo na hilo?
 
Hata mie nimeulizia leo asubuhi nikaambiwa halijatoka. nikanunua MwanaHalisi. sasa hivi nasikia nao wanatakiwa watoe maelezo kwa Serikali kutokana na habari iliyo ndani ya gazeti hilo isemayo 'Njama Kumng'oa Kikwete Zafichuka' mwandishi Saed Kubenea. kazi kwelikweli...
 
Raia Mwema limeshindwa kuingia mitaani kutokana na tatizo la mitambo ya kuchapiusha. hata Mtanzania zimeingizwa mitaani nakala chache sana. nasikia na magazeti mengi ya Shigongo nayo yameathirika.
Hiyo barua ya serikali kwa MwanaHalisi hata mimi nimeiona, kweli Mhariri anatakiwa kujielezea kutokana na habari yake kuu ya leo kuwa kuna njama za kumng'oa kikwete na mwanawe, Riz, anahusika
 
Nimeongea na mmoja wa wakurugenzi amesema gazeti litatoka kesho. Tusubiri tuone.
 
raia mwema arusha tumelisoma na nimelinunua muda wa saa tisa hivi wakati nimetoka ofice kwa ajili ya mizunguko nikalikuta mitaani.
 
raia mwema arusha tumelisoma na nimelinunua muda wa saa tisa hivi wakati nimetoka ofice kwa ajili ya mizunguko nikalikuta mitaani.

nadhani walichapakopi chache zambazo wamezipelekwa katika baadhi ya mikoa
 
yeah wameniambia kuwa walichapisha nakala za mikoani, ilipokuja suala la Dar, ndio kukawa na tatizo. Hivyo watu wa mikoano watakuwa wamelipata.
 
hapa mbeya tulilipata kama kawaida, na habari za leo ni kama , ufisadi, siasa, mzizi wa fitina kwa walimu, ccm,cuf, chadema wahusika,

mizengwe ziara ya kikwete mbeya, tarime yatikisika nk
 
Baada ya kutoka na habari motomoto wiki iliyopita (Safari za JK Utata) na nyingine nzito, nimeamka nikikutana na email kibao za watu wakiuliza "Raia Mwema iko wapi". Je kumekuwa na upungufu wa uchapishaji, halikutoka kama imetarajiwa au litatoka late?

Mchuuzi mmoja amedai waliambiwa watapata mchana na sasa ni jioni hawajaliona, Have you seen Raia Mwema today?

Mheshimiwa,

nitawezaji kukipata hicho kijarida? niko mbali na wachuuza magazeti lakini mtandao umenifikia, km uonavyo.
 
Back
Top Bottom