Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Baadhi ya Raia nchini Burkina Faso wameanzisha utaratibu wa kutumia muda wa usiku katika barabara na maeneo muhimu ya mji mkuu wa Ouagadougou badala ya kulala majumbani mwao ili kumlinda Rais Kapteni Ibrahim Traore dhidi ya jaribio lolote la mapinduzi.
Raia hao walioanzisha kikundi kinachoitwa Les Wayiyans, kwa miaka miwili tangu 2022 Rais Ibrahim Traore alipoingia madarakani kwa njia ya mapinduzi,wamekacha vitanda vyao na kujitolea kuwa sehemu ya ulinzi wa Rais.
Inapofika nyakati za usiku, raia hao hukutana pamoja kisha kugawanyika katika vikundi mbalimbali vinavyoenda kulinda maeneo mbalimbali mfano barabara ya kuelekea ikulu, redio ya taifa, uwanja wa ndege n.k.
Wanapokuwa katika maeneo hayo, huwasiliana kwa njia mbalimbali kama vile Whatsapp na pale kikundi chochote kinapohisi hatari yoyote hutoa taarifa kwa vikundi vingine pamoja na kwa maafisa wa usalama wa Burkina Faso.
Katika mahojiano, raia hao walisema wameamua kuchukua jukumu la kumlinda Kapteni Ibrahim Traore kwa sababu mbalimbali kama vile kuepuka yaliyomkuta Thomas Sankara yasimkute Ibrahim Traore, kutowaamini wanasiasa, kutoziamini nchi za Magharibi na kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Rais Ibrahim Traore kurejesha usalama nchini Burkina Faso.
Vilevile Raia hao walisema wataendelea kujitolea kumlinda Rais Ibrahim Traore hadi hapo watakapojiridhisha kuwa hakuna kitisho chochote cha usalama dhidi ya Rais Traore msisitizo ikiwa ni " kabla yeyote mwenye nia mbaya hajamfikia Ibrahim Traore,lazima apite kwao kwanza"
Source: