Raia wa Nigeria na Cameroon wakamatwa na mashine ya kuchapisha Pesa Bandia

Raia wa Nigeria na Cameroon wakamatwa na mashine ya kuchapisha Pesa Bandia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Maofisa Uhamiaji mkoa wa Pwani wamewakamata raia wawili wa Afrika Magharibi wakiwa na karatasi za kuchapisha pesa bandia, kemikali na kasiki (safe) la kutunzia fedha.

Watu hao wamekutwa pia na hati za kusafiria 34 za nchi za Nigeria na Ghana.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo, Abubakar Kunenge, amewataja watu hao waliokamatwa eneo la Mapinga, Bagamoyo, kuwa ni Livingstone Ese Onayomake (raia wa Nigeria) na Bertrand Noubissie (raia wa Cameroon).

Kunenge amesema Februari 9, 2023 walipokea taarifa za kiintelijensia kuhusu watu wanaotiliwa mashaka na siku iliyofuata ulifanyika upekuzi na kuwakamata raia hao.
Amesema wakati wa upekuzi mtuhumiwa Onayomake alikutwa na paspoti 34 ambazo si zake, kati yake 32 ni za Nigeria na mbili za Ghana.

Kunenge alisema alipohojiwa, mnaijeria huyo alidai alichukua paspoti hizo kwa lengo la kuwatafutia wahusika viza ya Uturuki.

"Jambo la kusikitisha raia hao walikutwa wakihifadhiwa na mtanzania, na mbaya zaidi mmoja alishaanza kujihusisha na utengenezaji wa fedha bandia maana alikutwa karatasi zilizoandaliwa kwa ajili ya kuchapisha noti bandia, kemikali pamoja na kasiki (safe) la kutunzia fedha,"alisema Kunenge.

Afisa uhamiaji Mkoani Pwani, Omary Hassan amesema baada ya kupata taarifa walienda kufanya upekuzi maungoni na kwenye makazi waliokua wakiishi.

Hassan ameeleza wahamiaji hao walikua wakiishi nyumbani kwa New Era Nyirembe ambaye alikua mke wa mtuhumiwa Noubissie, kwa sasa marehemu.

Amesema wamebaini kufuatia uchunguzi wa awali kuwa Onayomake aliingia nchini Februari 11 mwaka 2020 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupewa viza ya matembezi ya siku 90 hadi Mei 05 mwaka 2020 lakini baada ya hapo ameendelea kuishi nchini kinyume na sheria hadi alipokamatwa.

"Kuhusu Noubissie raia wa Cameroon yeye amekutwa na paspoti yenye namba 0441270 iliyotolewa Cameroon April 12, 2016 na iliisha muda Aprili 12 2021 na aliingia nchini mara ya mwisho Novemba 2, 2019 kupitia uwanja huo huo na alipewa viza ya matembezi iliyoisha Februari 01, 2020," amesema Hassan.

Kufuatia tukio hilo, Kunenge ametoa rai kwa wananchi mkoani Pwani kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi waonapo watu wanaowatilia mashaka.

Pia amewataka raia wa kigeni kuhakikisha uwepo wao nchini unazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

MWANANCHI
 
Hawa wanachofanyaga ni kujifanya wanatengeneza pesa ili sio kuchapisha kuziingiza kwenye mzunguko.

Yani huwa wanatafuta mafamba wanawadanganya kuwa ukileta milion 1 tunakuzalishia milion moja nyngne, na mara ya kwanza unaweza leta wakakupatia ukajaa ukaleta nyingi hapo ndo umepigwa sasa.

Na passport huwa wanakuwa na watu wao wanazikusanya wanaenda gongewa mihuri ionekane walitoka wakarudi.

Wawest wana michezo mingi ya kitapeli sana hapa mjini
 
Jamaa wamenusa fursa kwamba kuna uhaba wa pesa hapa bongolala, wakaja na mradi wa kuchapisha pesa....
 
Kesho tu tutasikia wametoroka gerezani na kukimbia nchi. Hii nchi ina mambo ya ajabu sana.

Sio kweli, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
Yaani hao watasota gerezani mpaka waone cha moto, si unamkumbuka yule manigeria wa madawa aliye fia Segerea na mzungu mwingine alikufa na corona Keko!
Askari wetu wako imara sana na watu kutoka nje!
Chezea Tanzania [emoji1241] utajikuta unachezwa wewe!
 
Sio kweli, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
Yaani hao watasota gerezani mpaka waone cha moto, si unamkumbuka yule manigeria wa madawa aliye fia Segerea na mzungu mwingine alikufa na corona Keko!
Askari wetu wako imara sana na watu kutoka nje!
Chezea Tanzania [emoji1241] utajikuta unachezwa wewe!
Wakati tuliambiwa Mnigeria katoroshwa tukazugwa kuwa kafa. Wapi kaburi lake?
 
Naomba kufahamu, hivi Uhamiaji wanapotoa hiyo visa ya matembezi ya siku 90 huwa hakuna tena ufuatiliaji kama mhusika ametoka nchini? Au inakuwaje
Mgeni anapoingia; kwa mfano; pale airport, atalipa fedha, kujaza fomu inayoonyesha anashukia wapi na anakaa muda gani. Mara nyingi hugongewa visa ya siku 90 kwenye passport yake. Akishagongewa yuko huru kuingia mitaani. Siku alizopewa zikiisha bila kuondoka, itakuwa ngumu uhamiaji kujua yuko wapi na anafanya nini japo rekodi zao zitaonyesha kuwa hajatoka. Ni mpaka pale atakapotoka ndiyo atakatwa kwa kupitiliza siku. Au Labda akiwa mtaani afanye kosa akamatwe, au aulizwe kitambulisho na polisi. Hili tatizo la visa kuisha na wageni kutoondoka ni tatizo kubwa na lipo kila nchi. Mgeni ni rahisi sana kujificha mapaka ije itokee ajali ya kukamatwa kwa uhalifu, au aulizwe kitambulisho kwa kuhisiwa etc...
 
Back
Top Bottom