Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Uingereza yaanza kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa tatu chini ya miaka mitano.
Uchaguzi huu, ambao ni wa kwanza kufanyika mwezi Disemba karibia miaka 100, unafuata ule uliotangulia ndani ya miaka ya 2015 na 2017.
Vituo vya kupiga kura ndani ya maeneo 650 kutoka Uingereza, Wales, Uskochi na kaskazini mwa Ireland vimefunguliwa leo kuanzia saa 07:00 asubuhi GMT.
Kura zitaanza kuhesabiwa saa 22:00 usiku GMT, mara baada ya vituo kufungwa. Matokeo mengi yanatarijiwa kutangazwa katika masaa ya mapema ya Ijumaa asubuhi.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa kwa kutumia mfumo wa 'first-past-the-post' unaotumika kwenye uchaguzi mkuu, ambao wapiga kura huchagua yule wanayemtaka, na mgombea atakayepata kura nyingi zaidi ndiye atakaeibuka mshindi.
Mwaka 2017, Newcastle ya kati ilikuwa ya kwanza kumaliza kuhesabu kura na kutangaza matokeo saa moja baada ya vituo kufungwa.
Kwa kawaida uchaguzi nchini Uingereza hufanyika kila baada ya miaka minne au mitano.
Lakini mwezi Oktoba. Wabunge walipgira kura kutaka uchaguzi wa pili ufanyike baada ya miaka mingi sana. Ni uchaguzi wa kwanza kufanyika msimu wa baridi tangu mwaka 1974 na wa kwanza kufanyika mwezi Disemba tangu mwaka 1923.
Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 na zaidi anaruhusiwa kupiga kura, ikiwa ni raia wa Uingereza au raia halisi wa nchi za jumuiya ya madola au Umoja wa Ireland na wamejiandikisha kupiga kura.
Kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kulifungwa tarehe 26 Novemba.
Maelezo kuhusu sehemu za kupiga kura yanaweza kupatikana katika tovuti ya tume ya uchaguzi na pia yameorodheshwa katika kadi zinazotumwa kwenya nyumba za watu.
Watu hawahitaji kadi ya kupiga kura ili kuweza kupiga kura lakini watahitajika kutoa majina yao na anuani zao katika vituo vya kupiga kura.
Watu wanaruhusiwa kumpigia kura mgombea mmoja tu lasivyo kura zao hazitohesabiwa.
Mbele ya uchaguzi huu, waangalizi wamewakumbusha raia kuwa hawaruhusiwi kupiga picha aina ya selfie ndani ya vituo vya kupiga kura na inaweza kuwa ni uvunjaji wa sheria.
Watu wengi wameshaweka alama ya kosa pembezoni mwa mgombea wanayempenda kwa kupiga kura kwa njia ya anuani.
Zaidi ya watu milioni saba walipiga kura kwa kutumia njia ya anuani miaka miwili iliyopita.
Wale waliojiandikisha kupiga kura kwa njia ya anuani lakini bado hawajarudisha kadi yao kwenye ofisi za uchaguzi, wanatakiwa kurudisha leo kabla ya 22:00 usiku GMT.
Pia wanaweza kupeleka kadi zao katika vituo vyao vya karibu vya kupiga kura, ikiwa kama njia mbadala.