John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Maelfu ya raia wa Ukraine wamevuka mipaka kuingia katika mataifa jirani katika upande wa Magharibi kutafuta usalama, wakati Urusi ikishambulia mji mkuu wa nchi hiyo pamoja na miji mingine kwa mashambulizi ya angani.
Wengi wa waliowasili katika mataifa hayo jirani ni wanawake, watoto na wazee baada ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy siku ya Alhamisi kuwapiga marufuku wanaume wa umri wa kujiunga na jeshi kuondoka nchini humo.
Mwanamke mmoja kutoka Mji Mkuu Kyiv aliyewasili Mjini Przemsyl, Poland aliangua kilio alipokuwa akielezea jinsi wanaume walivyoshukishwa katika treni nchini Ukraine kabla ya kufika katika eneo la mpaka.
Hapo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi alisema zaidi ya wakimbizi elfu 50 wa Ukraine wametoroka nchi hiyo katika muda wa chini ya saa 48 huku wengine wakiendelea kuelekea katika maeneo ya mpakani. Grandi amesema wengi wamekimbilia Poland na Moldova.
Source: DW