Raia walia na hali ngumu ya maisha chini ya Rais Tinubu

Raia walia na hali ngumu ya maisha chini ya Rais Tinubu

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
15 FEBRUARY 2024
Kano City, Jimbo la Kano
Nigeria

WATAASI RAIA, HALI NGUMU YA MAISHA KASKAZINI, WAMECHOKA AHADI ZETU VIONGOZI



Watuma ujumbe mzito, raia sasa wagombania makabi ya mpunga badala ya mchele kutokana na ughali wa maisha na kumtahadharisha mheshimiwa rais Bola Ahmed Adekunle Tinubu..

Mfano jimbo la Kano utakutana na foleni ndefu za kinamama wakisuburi kupewa misaada ya vibaba vya nafaka toka misikitini na kwa wasamaria wema wenye uwezo.

Kila kona ya nchi kuna dalili ya njaa kali, umasikini na ughali wa maisha iopitiliza kiasi watu hawawezi kula mlo mmoja kwa siku bila kuhangaika sana .

Watu wavamia machine za kukoboa mpunga kukusanya makapi wakapike chakula badala ya kwenda sokoni au dukani kwani mambo yamekuwa magumu sana.

Na huko Kaduna pia viongozi wa kijamii kamaMuhammad Abubakar III, Sultani wa Sokoto, amelalamikia hali ngumu ya kiuchumi nchini humo akisema Wanigeria wana hasira na njaa.

Mtawala huyo wa kimila alizungumza katika mkutano wa 6 wa kamati kuu ya baraza la watawala wa jadi wa kaskazini (NTRC) ambao ulifanyika katika jimbo la Kaduna siku ya Jumatano.

Alisema ukosefu wa usalama na umaskini ndio masuala makuu yanayosababisha matatizo kwa watu wa kaskazini ya Nigeria.
1708045729110.png

Picha: Muhammad Abubakar III, Sultani wa Sokoto

" Mambo yanaendelea kuwa mabaya zaidi, tunakabiliwa na viwango vya kuongezeka kwa umaskini wa watu wetu wengi; ukosefu wa vyanzo vya kawaida vya kujikimu kwa mwananchi wa kawaida kupata hata mlo mzuri kwa siku,” alisema

"Lakini ninaamini kuzungumzia ukosefu wa usalama na kuongezeka kwa kiwango cha umaskini ni masuala mawili ambayo hatuwezi kukunja mikono yetu huku tukibweteka na kufikiri kila kitu kiko sawa.

"Nimesema mara nyingi sana na katika vikao vingi sana kwamba, mambo si sawa nchini Nigeria na bila shaka, mambo pia hayako sawa kaskazini.

“Kwangu mimi, serikali hii ni mwendelezo wa serikali ya zamani; ni chama kimoja

“Kwa hiyo, tatizo ni nini hasa? Nadhani hiyo ndiyo sababu mojawapo ya sisi kuwa hapa kuzungumza na sisi wenyewe.”

Sultani huyo alisema watawala wa kimila / jadi / machifu wana wajibu kwa Wanigeria, ambao wanaamini katika taasisi hiyo ya kitamaduni, kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayoikabili nchi hiyo.

"Elimu ni muhimu, hivyo suala lolote unalotaka kuleta hapa, lazima uzungumze kuhusu elimu, lazima uzungumzie masuala ya afya na yale madudu mawili ambayo yamekuwa yakitusumbua sote hapa ambayo ni ukosefu wa usalama na umasikini," alisema.

“Na tusiichukulie kuwa ya kawaida; watu wako kimya, wako kimya kwa sababu fulani kwa sababu watu wamekuwa wakizungumza nasi viongozi wa kijadi

Tumekuwa tukizungumza nao, tumekuwa tukijaribu kuwaambia wawe na subira mambo yatakuwa sawa na wanaendelea kuamini.

"Ila ninamuomba Mwenyezi Mungu kwamba hata siku moja raia hawataamka na kusema hatukuamini tena, kwa sababu hilo litakuwa shida kubwa kwa taifa sababu hatuwezi kuwanyamazisha watu hawa kama viongozi wa kimila, kiroho na wanadiplomasia milele.

“Tumefikia kiwango hicho, watu wamechafukwa sana mioyoni , watu wana njaa, wana hasira, lakini bado wanaamini kuna watu wanaweza kuzungumza nao, wanawaamini baadhi ya wakuu wao wa mikoa, watawala wengine wa kimila, na wengine wao. viongozi wa dini.

“Kwa bahati nzuri, baadhi yetu maradufu kama viongozi wa kimila na wa kidini.

"Kwa hivyo, tuna kazi hii nzito ya kuwafikia kila mtu, kuwapoza, kuwafariji, kuwatuliza, na kuwahakikishia mambo yatakuwa sawa, na wanapaswa kuendelea kusali na kusali na bado kufanya kitu kizuri kwa sababu maombi bila kazi hayataleta chochote."

Sultani Abubakar pia alielezea wasiwasi wake kuhusu kundi kubwa la mamilioni ya vijana wasio na ajira nchini Nigeria, akibainisha kuwa inaleta hatari kubwa kwa usalama, amani na utulivu wa nchi.

"Lazima tutafute ajira kwa vijana wetu waliojaa vijiweni ambao wamekaa bila kazi na nimesema mara nyingi sana, tunakaa juu ya pipa kubwa lililojaa la baruti, tukiwa na vijana waliozagaa katika mamilioni yao, bila kazi, bila chakula, tunatafuta shida." aliongeza.

Aliongeza kuwa baraza la viongozi wa jadi liko tayari kufanya kazi na magavana.

"Na kama magavana pia wanataka kuwa na amani na utulivu katika majimbo yao, lazima wafanye kazi na viongozi wa kimila," alisema.
 
RAIS TINUBU AREJEA TOKA ZIARA BINAFSI YA SIKU KUMI NA TATU PARIS UFARANSA NA KUTOA TAMKO JUU YA MKAKATI KUPAMBANA NA GHARAMA ZA MAISHA


View: https://m.youtube.com/watch?v=Ipv8EZUGe6Q

Baada ya kukaa kwa siku 13 huko Paris, Ufaransa, Rais Bola Tinubu amerejea Nigeria kutoka kwa ziara yake ya kibinafsi.

Rais, ambaye aliondoka Abuja Januari 24, alikaribishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe, Abuja Jumanne jioni na maafisa wakuu wa serikali.
1708077387324.png

Rais Tinubu alikuwa katika ziara ya faragha nchini Ufaransa kulingana na taarifa ya msemaji lakini taarifa hiyo haikutoa maelezo kuhusiana na madhumuni ya ziara hiyo.

Kurejea kwake toka ziara binafsi ndefu kunakuja huku kukiwa na ongezeko la wasi wasi juu ya gharama ya maisha, ikichochewa na maandamano katika baadhi ya majimbo.

Zaidi ya hayo, vyama vya upinzani, makundi ya kijamii na kiutamaduni, na mashirika ya kiraia yameonyesha kutofurahishwa na kutokuwepo kwake, hasa katika kukabiliana na ongezeko la visa vya utekaji nyara na changamoto nyingine za usalama nchini Nigeria.

Adesuwa Omoruan
 
Niger state,
Nigeria

Wakaazi wa jimbo la Niger nchini Nigeria waandamana kutokana na gharama za maisha kuwa juu


View: https://m.youtube.com/watch?v=1z2A_jxMc1s&pp=ygUbTmlnZXIgc3RhdGUgY29zdCBvZiBsaXZpbmcg

Watu wapinga taarifa ya serikali kuwa gharama za maisha nchini Nigeria ni za chini kulinganisha na nchi zote za kiAfrika, hivyo ni himilivu. Lakini wananchi wanalia njaa huku hawana kipato cha kulisha familia zao wamesema raia walipohojiwa ...

Jimbo la Niger ni kubwa kwa eneo kuliko majimbo mengine ya nchini Nigeria ...
 
21 February 2024

Idara ya ushuru (Customs) ya Nigeria kuachia vyakula ilivyokamata vya magendo kunusuru njaa Nigeria

1708595806383.png

The Nigeria Customs Service (NCS) has expressed its readiness to distribute seized food items to Nigerians to help mitigate the current hardship in the land.

It said the distribution would be done after all the food items have been certified fit for human consumption.

The service National Public Relations, CSC Abdullahi Maiwada, in a statement, issued on Tuesday, said through the action the Comptroller General is reaffirming his commitment to advancing President Bola Ahmed Tinubu’s food security agenda.
 
06 August 2024
Nigeria

NJAA, UMASIKINI, UFISADI WA VIONGOZI VINACHOCHEA MAANDAMANO, WATAWALA WASIKILIZE SAUTI ZA WAANDAMANAJI

Mwanaharakati wa Haki za Kibinadamu na mbunge wa zamani, Bw. Shehu Sani ametoa wito kwa viongozi wa kaskazini mwa Nigeria kuja pamoja kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili eneo hilo ili amani itawale. Mbunge huyo wa zamani alisema amani haiwezi kutawala katika eneo hilo ikiwa wasomi na viongozi wa kisiasa wataendelea...


View: https://m.youtube.com/watch?v=PFkSixPEHUI

bendera za Russia zapeperushwa na waandamanaji mjini Kaduna kuashiria wanataka mapinduzi ya kijeshi kama yale ya nchini za Mali, Guinea, Burkina Faso, Niger na kwingine yafanyike Nigeria....

Human Rights activist and a former lawmaker, Shehu Sani has appealed to leaders in the northern Nigeria to come together an address economic challenges facing the region for peace to reign. The former lawmaker said peace may not reign in the region if the elites and political leaders continue to...
 
bendera za Russia zapeperushwa na waandamanaji mjini Kaduna kuashiria wanataka mapinduzi ya kijeshi kama yale ya nchini za Mali, Guinea, Burkina Faso, Niger na kwingine yafanyike Nigeria....

06 August 2024
Abuja, Nigeria

MAMBO MAZITO VIONGOZI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WAONGEA NA MEDIA
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi wajitokeza ktk kituo cha televisheni tajwa.

Viongozi hao ni mkuu wa utawala jeshini (Chief of Staff) wa Jeshi la Ulinzi la Nigeria, IGP wa Polisi, Commissioner wa Uhamiaji, Mkurugenzi wa Usalama wa Umma DSS na Commissioner wa Nigeria Customs


1722978104961.png

Wazungumza mazito, waomba waandamanaji wasifanye vurugu, pia watambue kubeba bendera ya nchi ya kigeni ni kosa la kihaini.

Viongozi hao wazungumzia hali ya kiuchumi, ugumu wa maisha, upatikanaji chakula kwa bei nafuu na hivyo waomba wananchi wawe watulivu wakati serikali ikitafuta hatua za haraka kuwapatia wananchi nafuu ktk maeneo yanayowagusa ...
 
Kiuharisia,alifight kupata cheo,ila kwa umri ule,hana msaada wowote kwa taifa
 
06 August 2024

Air Marshal Hasan Bala Abubakar - Maandamano Yametufanya Kuongea Na Vyombo Vya Habari

azungumza muda huu, asema akazia kuwa ni haki kuandamana lakini bila vurugu au kuonesha uhaini kwa kubeba bendera za Russia

1722978983720.png

Viongozi wazungumzia hali ya kisiasa, kijamii, demokrasia na uhuru wa kuchagua viongozi waatakao kupitia uchaguzi

Ila maandamano yanayoendelea kudai nchi ipinduliwe na kutamani nchi ya kigeni iingilie katika na kupindua serikali ya Nigeria ... tupo tayari kulinda hilo lisitokee...
 
06 August 2024

JESHI LIPO KULINDA DEMOKRASIA

Mkuu wa Utawala jeshi la Nigeria, Meja Jenerali Taoreed Lagbaja amesema jeshi la Nigeria lina matumaini kwamba taifa hilo halitaingia katika machafuko ambayo yatahitaji kuingilia kati...



View: https://m.youtube.com/watch?v=zO2PeE_h-fg

The Chief of Army Staff, Major General Taoreed Lagbaja has said the Nigerian army is hopeful the nationwide will not degenerate into anarchy that will require their intervention...
 
06 August 2024

JESHI LIPO KULINDA DEMOKASIA

Mkuu wa Utawala jeshi la Nigeria, Meja Jenerali Taoreed Lagbaja amesema jeshi la Nigeria lina matumaini kwamba taifa hilo halitaingia katika machafuko ambayo yatahitaji kuingilia kati...



View: https://m.youtube.com/watch?v=zO2PeE_h-fg

The Chief of Army Staff, Major General Taoreed Lagbaja has said the Nigerian army is hopeful the nationwide will not degenerate into anarchy that will require their intervention...

Kama Tinubu na serikali yake haitapata suluhu ya mambo yanayoendelea basi likely hood ya jeshi kushika hatamu ni kubwa
 
Kama Tinubu na serikali yake haitapata suluhu ya mambo yanayoendelea basi likely hood ya jeshi kushika hatamu ni kubwa

Wananchi nchini Nigeria tayari wana ona dalili hizo.
1723015076991.png

Huku kukiwa na maandamano ya njaa yanayoendelea katika maeneo tofauti ya nchi, jeshi la Nigeria limeapa kuchukua hatua iwapo mambo yatazidi kuwa mbaya.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Abuja siku ya Ijumaa, Jenerali Christopher Musa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, CDS, alitaja uporaji unaoendelea, kupoteza maisha na uharibifu wa mali kuwa "ukichaa".

Jeshi kuanza kuchanganua matatizo ya nchi kupitia televisheni, huku likiunga haki ya maandamano kikatiba, rais Tinubu ambaye ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ni kama vile ametekwa nyara .

Muda utatuambia kama jeshi hawataingia tamaa kuingoza nchi hii ya Nigeria, yenye historia ya Mapinduzi kwa kisingizio uongozi wa kiraia umeshindwa kuongoza nchi kipindi cha sasa.
 
Safi hawa wanigeria wanakumbatia sanaa watu wa West ndio maana mpk raia wanabeba bendera ya urussi
 
Back
Top Bottom