SoC04 Raia wanapaswa kufundishwa sheria kama wanasisitiziwa wajibu

SoC04 Raia wanapaswa kufundishwa sheria kama wanasisitiziwa wajibu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
TANZANIA TUNAYOITAKA NI ILE AMBAYO RAIA WANAIJUA SHERIA KAMA WANAVYOJUA WAJIBU WAO.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukihangaika na matokeo ya ukiukwaji na upindishwaji wa sheria bila kupambana na mzizi wa haya yote ambao ni kutoijua sheria yenyewe.

Mfumo wetu wa elimu (tukiangazia somo la uraia) ambalo hufundishwa kuanzia ngazi ya awali mpaka kidato cha sita (kama general study) limeegemea kwenye upande mmoja wa kufundisha historia,kazi ya mihimili mitatu (bunge,baraza na mahakama) na sio haki na wajibu wa raia kulingana na katiba ya nchi.

Sheria imebaki kuwa ni mali ya watunga sheria(bunge) ,watumia sheria (mahakama) na wasimamizi wa sheria (vikosi vya ulinzi na usalama) na sio raia ambao sheria hizo zinatekelezwa juu yao.

Tumelifanyakuwa ni jambo la kawaida japo ni aibu kubwa kwa asilimia kubwa ya wahitimu hata wa ngazi ya juu ya masomo kushindwa kujua vifungu hata viwili vya sheria na haki zao kwenye katiba.

Swala la kujua sheria tunaamini ni jukumu la wanasheria na majaji.

Tunapaswa kufanyaje?
Mfumo wa elimu unapaswa kubadilika na kuongezwa kama sio kubadilishwa somo kuwa 'uraia na katiba' ambapo wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza haki zao kuanzia ngazi ya awali.

Serikali inapaswa kutenga fungu kubwa ili kufanya semina mbalimbali sehemu za kazi na makazi,kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kufundisha raia wake haki zao kama inavyofanya kwa wajibu wao
 
Upvote 0
Back
Top Bottom