Raila aelezea matumaini kushinda kesi yake mahakamani

Raila aelezea matumaini kushinda kesi yake mahakamani

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Raila1-800x445.jpg

Kiongozi wa muungano wa NASA- Raila Odinga ameelezea matumaini yake ya kushinda katika kesi aliyo-wasilisha katika Mahakama ya juu kupinga uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu tarehe 8 mwezi Augosti. Raila amesema kuna kila sababu ya kuamini ushahidi utakaowasilishwa na upinzani mbele ya Ma-jaji saba wa mahakama ya juu, unatosha kwa mahakama kukubaliana na hoja zake.

Akiongea jana baada ya kuhudhuria Ibada ya Jumapili kwenye kanisa la All Saints Cathedral Jijini Nairobi, kiongozi huyo wa NASA aliyeandana na vinara wenza, Kalonzo Musyoka na Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula, alisema azma ya upinzani kushika hatamu za uongozi wa taifa ingalipo.

Wakati huo huo, Polisi hapo jana walikatalia mbali ombi la muungano wa upinzani, NASA kuandaa maombi nje ya mahakama ya juu. Kamanda wa Polisi Jijini Nairobi, Japheth Koome alisema jambo hilo halitawezekana, kutokana na sababu za kiusalama.

Polisi waliimarisha usalama nje ya Jumba la mahakama ya Juu na pia katika maeneo yaliyo karibu, huku Ma-jaji saba wakipanga kusikiza kesi iliyowasilishwa na muungano wa NASA, kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais kuanzia saa tatu asubuhi hivio leo.

CHANZO: Radio Taifa
 
Atakuwa anaota.....kuruhusiwa kuingvia kwenye system ni hatua moja tuu lakini kuthibitisha kuibiwa ni hatua nyingine........
 
Sijui kwa kweli kama atashinda maana hoja zote za NASA zimepanguliwa na mawakili wa IEBC.
 
Kama kweli jinsi hoja za Nasa zilivyopanguliwa jana nina wasiwasi sana na ushahindi wao wa incubator president...maana jana hakuna hoja iliyokosa jibu...the game is on
 
Back
Top Bottom